Karibu kwenye Wikipedia,
kamusi elezo huru, kila mtu anaweza kuihariri!
Hadi leo tuna makala takriban 34,618 kwa Kiswahili
 • Biografia
 • Dini
 • Hisabati
 • Historia
 • Jiografia
 • Jamii
 • Jumuia
 • Lugha
 • Sanaa
 • Sayansi
 • Teknolojia
 • Tiba
 • Ujenzi
     

     

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

 • ... kwamba Ngorongoro imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?
 • ... kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
 • ... kwamba McDonald Mariga ni mchezaji wa mpira kutoka Kenya ambaye anaichezea kilabu cha Parma.


 • Dana Elaine Owens (amezaliwa tar. 18 Machi, 1970), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Queen Latifah, ni rapa, mwigizaji, na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Kazi zake Queen Latifah katika muziki, filamu na televisheni zimepelekea kupata tuzo ya Golden Globe, Screen Actors Guild Awards mbili, Image Awards mbili, Grammy Award, amechaguliwa mara sita kwenye Grammy, na kuchaguliwa tena kwenye Emmy Award na Academy Award.

  Latifah alizaliwa na kukulia mjini Newark, New Jersey, binti wa Rita, mwalimu wa shule ambaye alifanya kazi katika shule ya Irvington High School ya mjini New Jersey, na Lancelot Owens, Sr, ambaye ni afisa wa polisi. Wazazi wake walitalikiana wakati Latifah akiwa na umri wa miaka kumi. Latifah alikulia katika kanisa la Kibaptist. Jina lake la kisanii, Latifah (لطيفة), maana yake "laini" na "mwanana" kwa Kiarabu, alipewa jina hilo na binamu yake wakati ana umri wa miaka minane. Daima msichana shupavu, urefu wa futi 5'10" wa Latifah alikuwa mtu wa mbele katika timu ya mpira wa kikapu ya shuleni kwake. Aliimba kipengele cha "Home" kutoka katika filamu ya muziki ya The Wiz katika mchezo wa kuigiza wa shuleni kwake. ►Soma zaidi


  Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.

  Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.

  Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.

  Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili

  • Idadi ya makala: 34,618
  • Idadi ya kurasa zote: 82,523 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
  • Idadi ya hariri: 1,027,518
  • Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 25,531
  • Idadi ya wakabidhi: 9
  • Idadi ya watumiaji hai: 44 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
  Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
  (fungua anwani kwa browser yako, badilisha "Mwanzo" kwa jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
  • na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
  (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)

  Jumuia za Wikimedia

  Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.
  Commons
  Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
  Meta-Wiki
  Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
  Wiktionary-logo.svg
  Wikamusi
  Kamusi na Tesauri
  Wikibooks-logo.png
  Wikitabu
  Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
  Wikiquote-logo-51px.png
  Wikidondoo
  Mkusanyiko wa Nukuu Huria
  Wikisource-logo.png
  Wikisource
  Nyaraka Huru na za Bure
  Wikispishi
  Kamusi ya Spishi
  Graduation cap.png
  Wikichuo
  Jumuia ya elimu
  Wikinews-logo.png
  Wikihabari
  Habari Huru na Bure
  This article is issued from Wikipedia - version of the 9/12/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.