Istanbul

Istanbul kwa macho ya ndege; juu iko Bahari Nyeusi, chini Bahai ya Marmara; sehemu ya Asia upande wa kulia, Ulaya upande wa kushoto wa Bospurus; "Pembe la dhahabu" ni mkono wa bahari unaoonekana chini upande wa Ulaya

Istanbul (kwa Kituruki unatajwa İstanbul) ni mji mkubwa zaidi katika nchi ya Uturuki, ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya milioni 11 na milioni 15, ambao wanaufanya kuwa miongoni mwa miji mikubwa ya dunia. Huu ndiyo mji mkuu wa Mkoa wa İstanbul.

Eneo la Istanbul linaelekea pande zote mbili za mlangobahari wa Bosporus unaotenganisha Ulaya na Asia. Hivyo ni mji wa pekee duniani uliopo katika mabara mawili.

Kiini cha kihistoria kipo upande wa Ulaya kwenye sehemu yenye umbo la rasi baina Bahari ya Marmara na Pembe la Dhahabu ambayo ni mkono wa bahari unaoingia ndani ya nchi na hivyo mahali pa mji ulikingwa kwa bahari pande tatu.

Historia

Mji huu umebadilisha jina lake mara kadhaa katika historia yake ya zaidi ya miaka 2600. Awali jiji hilo liliundwa mnamo mwaka 660 KK na Wagiriki kwa jina la Bizanti. Mnamo mwaka 330 BK Kaisari Konstantino aliufanya kuwa mji mkuu wa Dola la Roma akaupanua ukajulikana kama Konstantinopoli (yaani mji wa Konstantino).

Konstantinopoli uliendelea kama mji mkuu wa Dola la Roma na baadaye Roma ya Mashariki uliojulikana pia kama Milki ya Bizanti hadi 1453 ambako mji ulitwaliwa na Waturuki. Tangu mwaka ule uliendelea kama mji mkuu wa Milki ya Osmani hadi mwaka 1923. Baadaye serikali ya Uturuki ilihamia Ankara.

Wakati wa Waosmani majina mbalimbali yalitumiwa: Konstantinopoli au kwa kifupi "Konstantiniye", halafu tangu karne ya 18 pia "Istanbul". Tangu 1873 jina rasmi kwa Kituruki lilikuwa "Istanbul".

Kuwepo kwa bandari kumepelekea mji huo kuwa kitovu cha biashara katika Uturuki.

Katika Ukristo ni muhimu kama makao ya Askofu wa pili kwa heshima kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na mitaguso mikuu ya karne ya 4.

Hadi vita ya kwanza ya dunia Istanbul ilikuwa na wakazi wengi wakristo hasa Wagiriki na Waarmenia. Waarmenia waliteswa wakati ule wakapungua na baada ya vita Wakristo walibaguliwa kwa jumla kwa hiyo wengi walihamia Ugiriki. Leo hii Wagiriki waliobaki ni 2000 - 3000 pekee na Waarmenia ni takriban 50,000.

Majengo

Istanbul huwa na majengo mengi ya kihistoria kama vile

Kulingana na hadithi nyingi tofauti kuhusiana na KIZ KULESI, Constantine, Moja ya viongozi wa Byzantine alikuwa na binti yake ambaye inasemekana alikuwa mrembo sana ambaye alimpenda sana. Watabiri walitabiri kuwa kifo cha binti huyo kitatokana na kugonwa na nyoka. Katika kumlinda binti yake na janga hilo, mfalme akaagiza kujengwe nyumba katikati ya kisiwa ambapo ndipo Kiz Kulesi ilipo hivi sasa. Lakini mwisho wa siku Yule binti aliuawa kwa kugongwa na nyoka aliyekuja kisiwani kupitia katika kikapu cha mboga.

Elimu

Mjini Istanbul kuna vyuo vikuu mbalimbali, baadhi yao:

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Istanbul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
This article is issued from Wikipedia - version of the 4/22/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.