Alfabeti ya Kigiriki

Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko maalumu wa lugha ya Kigiriki. Herufi zake hutumiwa pia kama alama za kisayansi.

Historia

Alfabeti ya Kigiriki ilianzishwa wakati wa ustaarabu wa Ugiriki wa Kale na imeendelea kutumiwa hadi katika Ugiriki ya leo.

Ni alfabeti mama ya lugha za Ulaya, kwa sababu ni asili ya Alfabeti ya Kilatini ambayo ni mwandiko unaotumiwa zaidi duniani kushinda miandiko mingine. Ni pia asili ya alfabeti za Kikyrili na Kikopti. Kuna miandiko mingine ya kihistoria iliyotokana na Kigiriki.

Asili ya mwandiko huo ulikuwa alfabeti ya Kifinisia. Tofauti kubwa ni alama za vokali na baadaye badiliko la mwendo wa mwandiko kutoka kushoto kwenda kulia, tofauti na Kifinisia iliyoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto jinsi ilivyo hadi sasa katika mwandiko wa Kiarabu na wa Kiebrania ambazo ni lugha za Kisemiti jinsi ilivyokuwa Kifinisia.

Sehemu ya herufi zilizopokewa kutoka Kifinisia ziliachwa baadaye kwa sababu lugha haikuwa na sauti za kulingana nazo. Tangu mwaka 300 KK sehemu ya juu ya alfabeti inayoonyeshwa kwenye sanduku ilikuwa herufi za kawaida na alama za chini hazikutumiwa isipokuwa kama alama za namba.

Katika historia ndefu ya alfabeti hii matamshi ya alama yamebadilika pamoja na mabadiliko ya lugha yenyewe. Mwanafunzi wa Kigiriki cha Kale anayesoma maandiko ya Plato au vitabu vya Agano Jipya katika lugha asilia ataona matatizo akifika Ugiriki na kuwasikia Wagiriki wa leo: hata kama anaweza kusoma maandishi yote hataelewa mengi.

Matumizi ya namba

Kila herufi ilikuwa pia na matumizi kama tarakimu ya namba kwa sababu Wagiriki wa Kale hawakuwa na alama za pekee za namba. Herufi tatu za kihistoria ambazo hazikutumiwa tena kwa maandishi ziliendelea kama alama za namba yaani Wau au Stigma = 6 (alama ς), Heta = 8, San, Sho au Koppa = 90 (alama ϙ au ϟ) na Sampi = 900 (alama ͳ au ϡ au kama kwenye sanduku).

Kwa kutofautisha herufi na namba alama yake ilipewa mstari mdogo juu yake kama αʹ = 1, βʹ = 2, γʹ = 3. Kwa namba kuanzia 1,000 mstari upande wa kushoto uliongezwa, kwa mfano ͵α = 1,000, ͵β = 2000, ͵βηʹ = 2008.

Matumizi ya Kisayansi

Herufi za Kigriki zinatumiwa sana katika hesabu na sayansi. Mifano inayojulikana zaidi ni matumizi ya α, β na γ kama majina ya pembe za pembetatu.

Katika mahesabu ya duara namba π (pi) ni muhimu sana.

Kuna matumizi mengine mengi: karibu kila herufi ina maana fulani kisayansi.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alfabeti ya Kigiriki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 3/27/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.