Biolojia

ILANI: Kabla hujaendelea kuhariri makala hiyo, angalia malinganisho kati ya mapitio mawili yaliyopita na kuyaunganisha. Asante!

Biolojia ni sayansi asilia inayohusu utafiti wa uhai na viumbe hai, ikiwa ni pamoja na muundo wao, kazi, ukuaji, asili, mageuko, uenezi, na (nadharia ya) uainishaji.[1] Biolojia ni somo kubwa mno lenye vijisehemu, mada na masomo mengi. Miongoni mwa mada muhimu zaidi kuna kanuni tano unganishi ambazo zinasemekana kuwa misingi yenye hakika dhahiri ya biolojia ya kisasa:[2]

 1. Seli ni vitengo vya msingi vya uhai
 2. Spishi mpya na sifa bainishi za kurithiwa hutokana na mageuko
 3. Jeni ni vitengo vya msingi vya urithi
 4. Kiumbe kitadhibiti mazingira yake ya ndani kudumisha hali thabiti na imara
 5. Viumbe hai hula na kugeuza nishati.

Masomo madogo ya biolojia yanatumika kwenye msingi wa kipimo kinachotumiwa kufanya utafiti wa viumbe na mbinu zinazotumika kwa utafiti wao: biokemia huchunguza kemia isiyokomaa ya uhai; biolojia ya molekuli huchunguza kuathiriana changamani kwa mifumo ya biolojia ya molekuli, biolojia ya seli huchunguza kijenzi msingi cha maisha yote, seli; fiziolojia huchunguza shughuli za nje na za kemia za tishu, viungo, na mifumo ya viungo ya kiumbe hai; na ikolojia huchunguza jinsi viumbehai kadhaa huathiriana na kushirikiana na mazingira yao.[3]

Historia

"Mti wa Uzima" wa Ernst Haeckel (1879)

Neno biolojia katika maana yake ya kisasa linaonekana kuwa lilianzishwa na Karl Friedrich Burdach (1800), Gottfried Reinhold Treviranus (Biologie oder Philosophie der lebenden Natur, 1802), na Jean-Baptiste Lamarck (Hydrogéologie, 1802).[4][5] Ni mchanganyiko wa zamani wenye wahyi ya neno la Kigiriki βίος , bios, "uhai" na kiambishi tamati -λογία ,-logia, "utafiti wa."

Ingawa biolojia katika mtindo wake wa kisasa ni maendeleo ya hivi karibuni, sayansi zinazohusiana na zinazojumuishwa ndani yake zimechunguzwa tangu kale. Falsafa ya maumbile ilisomwa tangu siku za ustaarabu wa kale wa Mesopotamia, Misri, Bara Hindi na China.

Hata hivyo, asili ya biolojia ya kisasa na mtazamo wake kwa utafiti wa viumbe mara nyingi hupata asili yake kwa Ugiriki wa kale.[6] Huku mafunzo rasmi ya udaktari yakiwa yalianza wakati wa Hippokrates (460 KK hivi - 370 KK hivi), ni Aristotle (384 KK - 322 KK) ambaye alichangia sana ustawisho wa biolojia. Muhimu hasa ni "Historia ya Wanyama" na kazi zake nyingine ambazo alionyesha mwelekeo wa mwanaviumbe, na baadaye kazi za kijarabati zilizolenga usababisho wa kibiolojia na tofauti za uhai.

Theophrastus, mrithi wa Aristotle katika Lyceum, aliandika mfululizo wa vitabu juu ya botania ambavyo vilisalia kama mchango muhimu zaidi wa mambo ya kale kwa sayansi za mimea, hadi Karne za Kati.

Maendeleo muhimu katika utafiti na ustawisho wa biolojia yalikuzwa kwa juhudi za madaktari Waislamu kama vile msomi Mwafrika na Mwarabu al-Jahiz (781-869) katika zuolojia, [7]mwanabiolojia wa Kikurdi Al-Dinawari (828-896) katika botania,[8] na daktari wa Kiajemi Rhazes (865-925) katika anatomia na fiziolojia. Wanafalsafa hao walifafanua, kupanua, na kuboresha nadharia na utaratibu wa Kigiriki wa biolojia. Udaktari ulisomwa vizuri zaidi na wasomi wa Kiislamu waliofanya kazi katika mila za kifalsafa za Kigiriki, huku historia ya asili ikivutiwa sana na mawazo ya Aristotle, hasa katika kuunga mkono mfumo thabiti wa ngazi wa uhai.

Biolojia ilianza kuendelea na kukua haraka baada ya uboreshaji mkubwa wa darubini na Antony van Leeuwenhoek. Hapo ndipo wasomi waligundua manii bakteria, infusoria na ugeni tu na tofauti ya maisha ya hadubini. Uchunguzi wa Jan Swammerdam ulileta maslahi mapya katika entomolojia ikajenga mbinu za msingi za kuchangua na kutia madoa kwa hadubini.[9]

Maendeleo katika somo la hadubini pia yalikuwa na athari kubwa kwa kufikiri kibiolojia kwenyewe. Mapema katika karne ya 19, wanabiolojia kadhaa waliashiria umuhimu mkuu wa seli. miaka ya 1838 na 1839, Schleiden na Schwann walianza kuendeleza mawazo kuwa (1) kitengo muhimu cha viumbe ni seli na (2) seli za binafsi zina sifa zote bainifu za uhai, ingawa walipinga wazo kwamba (3) seli zote hutokana na mgawanyiko wa seli nyingine. Kwa msaada wa kazi ya Robert Remak na Rudolf Virchow, hata hivyo, katika miaka ya 1860 wanabiolojia wengi walikubali kanuni zote tatu za kile kilichojulikana kama nadharia ya seli.[10]

Wakati huohuo, taksonomia na uainishaji vikawa viini katika utafiti wa historia ya asili. Carolus Linnaeus alichapisha taksonomia ya msingi kwa ajili ya ulimwengu wa asili mwaka wa 1735 (mabadiliko yake yametumika tangu wakati huo), na miaka ya 1750 ilileta majina ya kisayansi ya spishi zake zote.[11] Georges-Louis Leclerc, Comte de Buffon, walielezea spishi kama vikundi bandia na viumbe hai kama vya kufulika - hata wakipendekeza uwezekano wa asili ya pamoja. Ingawa alikuwa anapinga mageuko, Buffon ni kielelezo muhimu katika historia ya mawazo ya mageuko; kazi yake ilishawishi nadharia za mageuko za Lamarck na Darwin.[12]

Mawazo makubwa ya mageuko yalitokana na kazi ya Jean-Baptiste Lamarck. Hata hivyo, ni mwanaviumbe Mwingereza Charles Darwin, akiunganisha mtazamo wa jiografia kama inavyoathiriwa na biolojia wa Humboldt, jiolojia ya kulingana ya Lyell, maandishi ya Thomas Malthus juu ya ukuaji wa idadi ya watu, na utaalamu wake mwenyewe wa kimofolojia, aliyeunda nadharia ya mageuko iliyokuwa na mafanikio zaidi iliyotokana na uteuzi asilia; mawazo sawa na ushahidi yalimfanya Alfred Russel Wallace kufikia uamuzi sawa.[13]

Ugunduzi wa uwakilishi wa kimwili wa urithi ulikuja pamoja na kanuni za mageuko na taaluma ya jenetiki inayohusu idadi ya watu. Katika miaka ya 1940 na mwanzoni mwa miaka ya 1950, majaribio yaliashiria kwa DNA kama sehemu ya kromosomu iliyoshikilia jeni. Kuzingatia viumbe vipya vya mfano kama vile virusi na bakteria, pamoja na ugunduzi muundo maradufu wa helikali wa DNA mwaka wa 1953, kuliashiria mpito kwa enzi ya jenetiki ya molekiuli.

Tangu miaka ya 1950 hadi sasa, biolojia imenyooshwa sana katika miliki ya molekiuli. Msimbo-jeni ulibanguliwa na Har Gobind Khorana, Robert W. Holley na Marshall Warren Nirenberg baada ya DNA kufahamika kuwa na kodoni.

Mwisho, Mradi wa Jenomu ya Binadamu ulianzishwa mwaka wa 1990 na lengo la kuwa na ramani ya jumla ya jenomu ya binadamu. Kimsingi, mradi huu ulikamilika mwaka wa 2003,[14] hata hivyo uchambuzi zaidi bado unachapishwa. Mradi wa Jenomu ya Binadamu ilikuwa hatua ya kwanza katika jitihada jumla za kushirikisha elimu iliyokusanywa ya biolojia katika fasili ya molekiuli ya kutenda ya mwili wa binadamu na miili ya viumbe vingine.

Misingi ya biolojia ya kisasa

Biolojia ya kisasa inaweza kujumuishwa ndani ya kanuni tano unganishi: nadharia ya seli, mageuko, usomi - jeni, homiostasisi, na nishati.[2]

Nadharia ya seli

Seli zinazokuza viini, madoa kwa keratini (nyekundu) na DNA (kijani)

Nadharia ya seli inasema kwamba seli ni kitengo cha msingi cha maisha, na kwamba viumbe vyote hai vimetengenezwa kwa seli moja au zaidi au bidhaa zinazotoka kwenye seli hizo (mfano kauri). Seli zote hutoka kwenye seli nyingine kupitia mtengo wa seli. Katika viumbe vyenye seli nyingi, kila seli katika mwili wa kiumbe hatimaye hutoka kwenye seli moja katika yai lililorutubishwa. Seli pia inazingatiwa kuwa kitengo cha msingi katika taratibu nyingi za patholojia.[15] Zaidi ya hayo, tukio la mtiririko wa nishati hutokea katika seli katika taratibu ambazo ni sehemu ya kazi inayojulikana kama umetaboli. Hatimaye, seli zina maelezo ya kurithiwa(DNA) ambayo hupitishwa kutoka seli hadi seli wakati wa mgawanyiko wa seli.

Mageuko

Uteuzi asilia wa idadi kwa mpangilio wa rangi wa giza.

Dhana kuu ya maandalizi katika biolojia ni kwamba maisha hubadilika na kukua kwa njia ya mageuko, na kwamba viumbe vyote hai vinayojulikana vina asili ya pamoja. Jean-Baptiste de Lamarck aliingiza mageuko kwenye msamiati wa kisayansi mwaka wa 1809, na[16] Charles Darwin akaithibitisha miaka hamsini baadaye kama nadharia yenye uwezo wa kujitegemea kwa kueleza msukumo wake kwa ufasaha: uteuzi asilia.[17][18] (Alfred Wallace Russel anatambuliwa kama mgunduzi mwenzi wa dhana hii kwa vile alisaidia kufanya utafiti na majaribio na dhana ya mageuko).[19] Mageuko sasa yanatumika kuelezea tofauti kubwa ya uhai unaopatikana duniani.

Darwin alitoa nadharia kwamba spishi na vizawa zilizo sitawisha kupitia taratibu za uteuzi asilia na uteuzi bandia au uzazi wa kuchagua.[20] Mfumko wa jeni ulikubaliwa kama utaratibu wa ziada wa usitawi wa mageuko katika usanisi wa kisasa wa nadharia.[21]

Historia ya mageuko ya spishi-inayoelezea sifa bainifu za spishi mbalimbali ambapo ilitoka-pamoja na uhusiano wake wa unasaba na kila spishi nyingine hujulikana kama filojeni yake. Mitazamo mbalimbali ya biolojia hutoa maelezo kuhusu filojeni. Haya ni pamoja na ulinganishi wa mfuatano wa DNA uliofanywa ndani ya biolojia ya molekiuli au usomi-jenomu, na ulinganishi wa visukuku au rekodi nyingine za viumbe wa kale katika paleontolojia.[22] Wana biolojia huandaa na kuchambua uhusiano wa mageuko kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na filojenetiki, fenetiki, na kladistiki. (Kwa muhtasari wa matukio muhimu katika mageuko ya maisha kama inavyoeleweka sasa na wana biolojia, angalia Muda wa mageuko.)

Nadharia ya mageuko inadai kwamba viumbe vyote duniani, vyote vinavyoishi na vilivyokufa, vilitoka kwa jadi moja au mrundiko wa jeni wa nasaba. Inaaminika kuwa huyu mhenga wa pamoja wa viumbe vyote alionekana miaka bilioni 3.5 iliyopita.[23] Kwa jumla, wana biolojia wanazingatia kilimwengu na kuenea pote kwa msimbo-jeni kama ushahidi wa hakika wa kuunga mkono nadharia ya asili ya pamoja ya bakteria zote, akea, na eukariyote (angalia: asili ya maisha).[24]

Usomi-jeni

Mraba wa Punnett ukifafanua kubadilishana kati ya mimea miwili ya punje zenye heterozigusi ya maua ya zambarau (B) na nyeupe (b)

Jeni ni vitengo vya msingi vya urithi katika viumbehai vyote. Jeni ni kitengo cha urithi na kinafanana na sehemu ya DNA inayoathiri umbo au kazi ya kiumbehai kwa njia maalum. Viumbehai vyote, kutoka kwa bakteria hadi kwa wanyama, hushiriki utaratibu sawa wa msingi unaonakili na kutafsiri DNA kuwa protini. Seli hunakili jeni ya DNA kuwa toleo la RNA la jeni, na kisha ribosomu hutafsiri RNA kuwa protini, mfuatano wa asidi amino. Msimbo wa tafsiri kutoka kodoni ya RNA hadi asidi amino ni sawa kwa viumbehai vingi, lakini tofauti kidogo kwa baadhi. Kwa mfano, mfuatano wa DNA unaosimba kwa insulini kwenye binadamu pia utasimba kwa insulini wakati unaingizwa katika viumbehai vingine, kama vile mimea.[25][26]

Kwa kawaida, DNA hutokea kama chromosomu ya mstari kwenye eukariyoti, na chromosomu mviringo katika prokariyoti. Chromosomu ni muundo wenye mpango unaojumuisha DNA na histoni. Seti ya chromosomu katika seli na maelezo mengine yoyote ya kurithiwa yanayopatikana katika mitokondria, chloroplasti, au maeneo mengine kwa pamoja yanajulikana kama jenomu yake. Kwenye eukariyoti, DNA ya jenomu iko katika kiini cha seli, pamoja na viasi vidogo katika mitochondria na chloroplasti. Katika prokariyoti, DNA imeshikiliwa ndani ya chembe cha kasoro kisicholingana katika sitoplazimu kiitwacho nyukliodi.[27] Maelezo ya jeni katika jenomu yanawekwa ndani ya jeni, na mkusanyiko kamili wa maelezo haya katika kiumbehai unaitwa aina-jeni yake.[28]

Homiostasisi

[[Picha:ACTH Negative Feedback.svg|right|thumb|250pc|Haipothalamasi hutoa CRH, ambayo huelekeza tezi ya pituitary kutoa ACTH. Kwa upande wake, ACTH huelekeza koteksi ya Adrena kutoa glukokotikoidi, kama vile kotisoli. Glukokotikoidi hupunguza kiwango cha utoaji wa ugiligili wa mwili wa haipothalamasi na tezi ya pituitary mara kiasi cha kutosha cha glukokotikoidi kinapotolewa. [29]

 • Epizoolojia - utafiti wa mambo yanayoathiri afya na magonjwa ya wanyama
 • Mikolojia - utafiti wa kuvu
 • Virolojia - utafiti wa virusi na baadhi ya vikolezo wengine wanaofanana na virusi

Tazama Pia

Picha

Tanbihi

 1. [3] ^ Kulingana na ufafanuzi kutoka Kamusi ya mradi wa Aquarena Wetlands.
 2. 1 2 Avila, Vernon L. (1995). Biology: Investigating life on earth. Boston: Jones and Bartlett, 11–18. ISBN 0-86720-942-9.
 3. [6] ^ Sayansi ya Maisha, Weber State Museum of Natural Science
 4. Junker Geschichte der Biologie, p8.
 5. Coleman, Biolojia katika karne ya kumi na tisa, pp 1-2.
 6. [12] ^ Magner, Historia ya Sayansi za Maisha
 7. [13] ^ Mehmet Bayrakdar, "Al-Jahiz And the Rise of Biological Evolutionism", The Islamic Quarterly, Third Quarter, 1983, London.
 8. Fahd, Toufic. "Botany and agriculture". p. 815. , katika (1996) Encyclopedia of the History of Arabic Science 3. Routledge. ISBN 0415124107.
 9. [17] ^ Magner, Historia ya Sayansi za Maisha, pp 133-144
 10. Sapp, Mwanzo, sura ya 7, Coleman, Biolojia katika karne ya kumi na tisa, sura ya 2
 11. [19] ^ Mayr, Ukuaji wa Mawazo ya Kibiolojia, sura ya 4
 12. [20] ^ Mayr, Ukuaji wa Mawazo ya Kibiolojia, sura ya 7
 13. [21] ^ Mayr, Ukuaji wa Mawazo ya Kibiolojia, sura ya 10: "Ushahidi wa Darwin wa mageuko na asili ya pamoja", na sura ya 11: "Sababu ya mageuko: uteuzi asilia"; Larson, Mageuko, sura ya 3
 14. BBC NEWS (2003-04-14). Iliwekwa mnamo 2006-07-22.
 15. Mazzarello, P (1999). "A unifying concept: the history of cell theory". Nature Cell Biology 1 (1): E13–E15. . .
 16. Packard, Alpheus Spring (1901). Lamarck, the founder of Evolution: his life and work with translations of his writings on organic evolution. New York: Longmans, Green.. ISBN 0405125623.
 17. [32] ^ Kazi kamili za Darwin kwenye Mtandao - Tawasifu. darwin-online.org.uk. Ilirejeshwa tarehe 15-12-2006.
  Dobzhansky 1973
 18. [34] ^ Kama msomi wa Darwin Joseph Carroll wa Chuo Kikuu cha Missouri-St. Louis anavyosema katika utangulizi wake wa uchapishaji upya wa kisasa wa kazi ya Darwin: "Mwanzo wa Spishi ni kazi tusiyoweza kuiasahau kwa urahisi. Ni moja ya kazi mbili au tatu muhimu zaidi maishani- moja ya kazi ambazo hubadilisha maono yetu ya dunia kimsingi na kwa kudumu.....Imejadiliwa kwa uthabiti mkali lakini pia ina lugha ya kushawishi, inaleta ubunifu, na ina balagha. " (2003) in Carroll, Joseph: On the origin of species by means of natural selection. Peterborough, Ontario: Broadview. ISBN 1551113376.
 19. [35] ^ Shermer ukurasa wa 149.
 20. Darwin, Charles (1859). Kuhusu Mwanzo wa Spishi, 1, John Murray
 21. Simpson, George Gaylord (1967). The Meaning of Evolution, Second, Yale University Press. ISBN 0300009526.
 22. [39] ^ Filojenia kwenye bio-medicine.org
 23. De Duve, Christian (2002). Life Evolving: Molecules, Mind, and Meaning. New York: Oxford University Press, 44. ISBN 0195156056.
 24. Futuyma, DJ (2005). Evolution. Sinauer Associates. ISBN 978-0878931873. OCLC 57311264 57638368 62621622.
 25. [45] ^ Kutoka SemBiosys, Aina Mpya ya Insulini NDANI YA WALL STREET ya Gene G. Marcial (13 Agosti 2007)
 26. http://www.i-sis.org.uk/gmSaffloweHumanPro-Insulin.php
 27. Thanbichler M, Wang S, Shapiro L (2005). "The bacterial nucleoid: a highly organized and dynamic structure". J Cell Biochem 96 (3): 506–21. . .
 28. [49] ^ Ufafanuzi wa Jenotaipu - Ufafanuzi wa Kamusi ya Uuguzi
 29. Raven, PH, Johnson, GB. Biolojia, Toleo la Tano, Boston: Hill Companies, Inc 1999. Ukarasa 1058 <. / REF>]] Homiostasisi ni uwezo wa mfumo wazi kudhibiti mazingira yake ya ndani kudumisha hali thabiti kupitia urekebishaji mwingi wa msawazo mwendo unaodhibitiwa na taratibu zinazohusiana za kanuni. Viumbehai vyote, kama vina seli moja au seli nyingi, hudhihirisha homiostasisi.<ref>[51] ^ Kelvin Rodolfo, [http://www.scientificamerican.com/article.cfm?id=what-is-homeostasis Maelezo ya Homiostasisi kwenye scientificamerican.com] . Ilirudishwa 16 Oktoba 2009.</ref> Ili kudumisha msawazo mwendo na kufanya kazi fulani kwa ufanisi, ni lazima mfumo wa ugundue na ujibu usumbufu. Baada ya kugundua usumbufu, kwa kawaida mfumo wa bayolojia utajibu kwa maoni hasi. Hii ina maana aidha kupunguza au kuongeza shughuli za kiungo au mfumo ili kudhibiti hali. Mfano mmoja ni kutoa glukagoni wakati viwango vya sukari ni vidogo mno.

  Nishati

  Muhtasari wa Msingi wa nishati na maisha ya binadamu.
  Maisha ya viumbehai yanategemea pembejeo isiosita ya nishati. Mmenyuko wa kemikali zenye wajibu wa muundo na kazi yake zimerekebishwa kutoa nishati kutoka kwenye dutu zinazofanya kazi kama chakula chake na kuzibadilisha kusaidia kuunda seli mpya na kuzihimili. Katika mchakato huu, molekiuli za dutu za kemikali zilizo na chakula huwa na kazi mbili, kwanza, zina nishati ambayo inaweza kubadilishwa kwa mmenyuko wa kibaiolojia wa kemikali; pili, zinakuza miundo mipya ya molekiuli iliyotengenezwa na biomolekiuli. Viumbe vyenye jukumu la kuingiza nishati katika mfumo ikolojia hujulikana kama wazalishaji au autotrofu. Karibu viumbehai hivi vyote huteka nishati kutoka kwa jua.<ref name="bryantfrigaard">{{cite journal | author = D.A. Bryant & N.-U. Frigaard |month=Novemba | year = 2006 | title = Prokaryotic photosynthesis and phototrophy illuminated | journal = Trends Microbiol | volume = 14 | issue = 11 | pages=488 | doi = 10.1016/j.tim.2006.09.001 | pmid = 16997562 | ref = harv }}</ref> Mimea na fototrofu nyingine hutumia nishati ya jua kupitia mchakato unaojulikana kama usanidinuru kubadili malighafi kuwa molekiuli ya ogani, kama vile ATP, yenye viunganishi vinavyoweza kuvunjwa kutoa nishati.<ref>{{cite book |author=Smith, A. L. |title=Oxford dictionary of biochemistry and molecular biology |publisher=Oxford University Press |location=Oxford [Oxfordshire] |year=1997 |pages=508 |isbn=0-19-854768-4 |quote=Photosynthesis - the synthesis by organisms of organic chemical compounds, esp. carbohydrates, from carbon dioxide using energy obtained from light rather than the oxidation of chemical compounds.}}</ref> Hata hivyo, mifumo ikolojia michache, hutegemea kabisa nishati iliyoondolewa na kemotrofu kutoka kwa methani, salfaidi, au chimbuko zingine zisizong'aa za nishati.<ref> Katrina Edwards. ''Mikrobiolojia ya Bwawa la Masimbi na Utiko ulio Mbichi, Baridi na wenye haidrolojia hai.'' Hydrologically Active Ridge Flank''Taasisi ya Taaluma ya Bahari ya Woods Hole.'' </ref> Baadhi ya nishati iliyopatikana hutumika kuzalisha uzitohai ili kuhimili maisha na kutoa nguvu kwa ajili ya ukuaji na usitawi. Nyinyi ya nishati hii inayosalia hupotea kama molekiuli za joto na taka. Michakato muhimu zaidi kwa kugeuza nishati iliyonaswa katika dutu za kemikali kuwa nishati muhimu kwa kuhimili maisha niumetaboli<ref>{{cite book |author=Campbell, Neil A. and Reece Jane B|title=Biology |publisher=Benjamin Cummings |year=2001 |chapter=6|isbn=978-0805366242 |accessdate= 2008 |oclc=47521441 48195194 53439122 55707478 64759228 79136407}}</ref> na upumuaji wa seli.<ref name="Colvard, 2009">[59] ^ Bartsch / ''Colvard, Mazingira Hai.'' (2009) Jarida la Prentice Hall Regents wa Jimbo la New York. Lilirudishwa tarehe 16 Oktoba 2009.</ref>

  Utafiti

  Muundo

  Mchoro wa mfano wa seli ya mnyama unaoonyesha organeli na miundo mbalimbali: 1. Nukleoli, 2. Kiini, 3. Ribosoma, 4. Vesikulo, 5. Retikulo isiyo laini plasmani, 6. Gimba la Golgi, 7. Kiunzi cha seli, 8. Retikulo laini plasmani, 9. Mitokondria, 10. Vakuolo, 11. Sitosoli, 12. Lisosoma, 13. Sentrioli.
  Biolojia ya molekiuli ni utafiti wa biolojia katika kiwango cha molekiuli.<ref>[61] ^ [http://www.biology-online.org/dictionary/Molecular_biology Biolojia ya Molekiuli - Ufafanuzi kutoka baiolojia-online.org]</ref> Uwanja huu wa kitaaluma unalingana na maeneo mengine ya biolojia, hasa na usoni-jeni na biokemia. Biolojia ya molekiuli inajihusisha hasa na kuelewa mwingiliano kati ya mifumo mbalimbali ya seli, ikiwa ni pamoja na uhusiano baina ya DNA, RNA, na usanisi wa protini na kujifunza jinsi mwingiliano huu unadhibitiwa. Biolojia ya seli inafanya utafiti wa sifa za muundo na za fiziolojia za seli, ikiwa ni pamoja na tabia zao, mahusiano, na mazingira. Hii hufanyika katika viwango vya hadubini na molekiuli, kwa viumbe vyenye seli moja kama vile bakteria pamoja na seli maalumu katika viumbe vyenye seli nyingi kama vile binadamu. Kuelewa muundo na kazi ya seli ni msingi kwa sayansi zote za biolojia. Mifanano na tofauti kati ya aina za seli ni muhimu hasa kwa biolojia ya molekiuli. Anatomia huzingatia maumo ya miundo yenye kuonekana kama vile viungo na mifumo ya viungo.<ref>[62] ^ [http://www.bartleby.com/107/1.html "Anatomia ya Mwili wa Binadamu."] toleo la 20. 1918. Henry Gray. </ref> Genetics ni sayansi ya jeni, urithi, na tofauti za viumbehai.<ref name="griffiths2000sect60">{{cite book |editor1-first=Anthony J. F. |editor1-last=Griffiths |editor2-first=Jeffrey H. |editor2-last=Miller |editor3-first=David T. |editor3-last=Suzuki |editor4-first=Richard C. |editor4-last=Lewontin |editor5-last=Gelbart |title=An Introduction to Genetic Analysis |year=2000 |isbn=0-7167-3520-2 |edition=7th |publisher=W. H. Freeman |location=New York |chapterurl=http://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/bv.fcgi?rid=iga.section.60 |chapter=Genetics and the Organism: Introduction |author=Anthony J. F. Griffiths .... |editor-first=William M.}}</ref><ref name="Hartl_and_Jones"> Hartl D, Jones E (2005) </ref> Jeni husimba maelezo muhimu kwa kusanisi protini, ambayo kwa upande mwingine huwa na jukumu kubwa katika kuathiri (ingawa, mara nyingi, si kuamua kabisa) fenotaipu ya mwisho ya kiumbehai. Katika utafiti wa kisasa, usomi-jeni hutoa nyenzo muhimu katika uchunguzi wa kazi ya jeni maalumu, au uchambuzi wa mwingiliano wa jeni. Ndani ya viumbehai, maelezo ya jeni kwa jumla hubebwa katika kromosomu, ambako yanawakilishwa katika muundo wa kemikali wa molekiuli hasa za DNA. Biolijia ya usitawi huchunguza utaratibu wa viumbehai wa kukua na kusitawi. Biolojia ya usitawi ya kisasa iliyopata asili yake katika embriolojia, huchunguza udhibiti wa jeni wa ukuaji wa seli, upambanuzi, na "mofojenesi," ambao ni utaratibu ambao ni chanzo cha tishu, viungo, na anatomia. Viumbehai mtindo vya biolojia ya usitawi ni pamoja na nematodi Caenorhabditis elegans, <ref>{{cite journal |author=Brenner, S. |year=1974 |month=Mei |url=http://dev.wormbase.org/papers/31_Brenner74.pdf |title=The Genetics of ''Caenorhabditis elegans'' |journal=[[Genetics (journal)|Genetics]] |volume=77 |pages=71–94|format=PDF |ref=harv}}</ref> nzi-tunda Drosophila melanogaster, <ref name="Encyclopedia of genetics">{{cite encyclopedia |last= |first= |author=James H. Sang |authorlink= |coauthors= |editor=Eric C. R. Reeve |encyclopedia=Encyclopedia of genetics |title=Drosophila melanogaster: The Fruit Fly |url=http://books.google.com.au/books?id=JjLWYKqehRsC&pg=PA157&lpg=PA157&dq=drosophila+eggs+day+lifetime&source=bl&ots=V5BTOFQFeh&sig=JYiRArLjNyJy8SJylcncC26hh08&hl=en&ei=wTtLSpPOF4nENrTSwLgC&sa=X&oi=book_result&ct=result&resnum=2 |accessdate=2009-07-01 |edition= |date=2001-06-23 |year= |publisher=Fitzroy Dearborn Publishers, I |volume= |location=USA |id= |doi= |pages=157 |quote= }}</ref> samakimilia Danio rerio, <ref>{{cite journal |title=Large scale genetics in a small vertebrate, the zebrafish |journal=Int. J. Dev. Biol. |volume=40 |pages=221–7 |year=1996 |pmid=8735932 |url=http://www.intjdevbiol.com/paper.php?doi=8735932 |author1=Haffter P |author2=Nüsslein-Volhard C |author-separator=, |issue=1 |ref=harv}}</ref> panya Mus musculus, <ref>{{cite journal |author=Keller G |title=Embryonic stem cell differentiation: emergence of a new era in biology and medicine |journal=Genes Dev. |volume=19 |issue=10 |pages=1129–55 |year=2005 |pmid=15905405 |url=http://genesdev.cshlp.org/content/19/10/1129.long |doi=10.1101/gad.1303605 |ref=harv}}</ref> , na gugu Arabidopsis thaliana. <ref>{{cite journal |author=Rensink WA, Buell CR |title=Arabidopsis to rice. Applying knowledge from a weed to enhance our understanding of a crop species |journal=Plant Physiol. |volume=135 |issue=2 |pages=622–9 |year=2004 |pmid=15208410 |doi=10.1104/pp.104.040170 |pmc=514098 |ref=harv}}</ref><ref>{{cite journal |author=Coelho SM, Peters AF, Charrier B, ''et al'' |title=Complex life cycles of multicellular eukaryotes: new approaches based on the use of model organisms |journal=Gene |volume=406 |issue=1-2 |pages=152–70 |year=2007 |pmid=17870254 |doi=10.1016/j.gene.2007.07.025 |ref=harv}}</ref> (Kiumbehai mtindo ni spishi inayochunguzwa sana kuelewa ishara maalum za biolojia, kwa matumaini kuwa uvumbuzi utakaofanywa katika kiumbehai hicho utatoa umaizi katika utendaji kazi wa viumbehai vingine).<ref>{{cite journal |author=Fields S, Johnston M |title=Cell biology. Whither model organism research? |journal=Science |volume=307 |issue=5717 |pages=1885–6 |year=2005 |month=Mar |pmid=15790833 |doi=10.1126/science.1108872 |url=http://www.sciencemag.org/cgi/content/summary/307/5717/1885 |ref=harv}}</ref>

  Fiziolojia

  Fiziolojia huchunguza utaratibu wa umakanika, kimwili, na wa biokemikali wa viumbehai kwa kujaribu kuelewa jinsi miundo yote hutenda kazi kama pamoja. Mada ya "muundo kwa kazi" ni kuu katika biolojia. Tangu jadi, utafiti wa fiziolojia umegawanyika katika fiziolojia ya mimea na fiziolojia ya wanyama, lakini baadhi ya kanuni za fiziolojia ni za kuenea pote, bila kuzingatia kiumbehai hasa kinachochunguzwaa. Kwa mfano, yale unayojifunza kuhusu fiziolojia ya seli za chachu yanaweza pia kutumika kwa seli za binadamu. Uwanja wa kitaaluma wa fiziolojia ya wanyama unaeneza zana na mbinu za fiziolojia ya binadamu hadi kwa spishi zisizo za binadamu. Fiziolojia ya mimea hukopa mbinu kutoka kwa maeneo yote ya utafiti. Fiziolojia huchunguza jinsi kwa mfano mifumo ya neva, kinga, endokrini, kupumua, na usambazaji inavyofanya kazi na kuathiriana. Uchunguzi wa mifumo hii unashirikiwa na taaluma zingine mahsusi za udaktari kama vile nyurolojia na elimu ya kingamaradhi.

  Mageuko

  Utafiti wa mageuko unahusu asili na ukoo wa spishi, ikiwa ni pamoja na mabadiliko yao baada ya muda, na inajumuisha wanasayansi kutoka taaluma zingine mahsusi za taksonomia. Kwa mfano, kwa jumla inahusisha wanasayansi wenye mafunzo maalum katika viumbehai hasa kama vile mammalojia, ornitholojia, botania, au herpetolojia, lakini hutumia viumbehai hivyo kama mifumo ya kujibu maswali ya kawaida kuhusu mageuko. Sehemu moja ya biolojia ya mageuko inategemea paleontolojia, ambayo inatumia kumbukumbu za kisukuku kujibu maswali kuhusu mtindo na mwendo wa mageuko,<ref name="Jablonski">{{cite journal |author=Jablonski D |title=The future of the fossil record |journal=Science |volume=284 |issue=5423 |pages=2114–16 |year=1999 |pmid=10381868 |doi=10.1126/science.284.5423.2114 |ref=harv }}</ref> na sehemu nyingine maendeleo katika taaluma kama viletaaluma ya jenetiki inayohusu idadi ya watu<ref>[83] ^ John H. Gillespie Usomi-Jeni wa Idadi: Mwongozo Mfupi, Johns Hopkins Press, 1998. ISBN 0-8018-5755-4.</ref> na nadharia ya mageuko. Katika miaka ya 1980, biolojia ya usitawi iliingia upya katika biolojia ya mageuko baada ya kutngwa hapo awali kutoka kwa usanisi wa kisasa kupitia utafiti wa biolojia ya maendeleo ya mageuko.<ref>[84] ^ Vassiliki Betta Smocovitis Biolojia ya Kuunganisha: usanisi wa mageuko na biolojia ya mageuko ISBN 0-691-03343-9.</ref> Nyuga zinazohusiana ambazo mara nyingi huzingatiwa kama sehemu ya baiolojia ya mageuko ni filojenetiki, utafiti wa mifumo, na taksonomia.

  Utafiti wa mifumo

  Bakteria Archaea Mnyama Kuvu Mmea
  A phylogenetic tree of all living things, based on rRNA gene data, showing the separation of the three domains bacteria, archaea, and eukaryotes as described initially by Carl Woese. Trees constructed with other genes are generally similar, although they may place some early-branching groups very differently, presumably owing to rapid rRNA evolution. The exact relationships of the three domains are still being debated.
  Matukio mbalimbali ya uibukaji wa spishi mpya huunda mfumo wenye muundo wa mti wa uhusiano kati ya spishi. Wajibu wa utafiti wa mifumo ni kuchunguza uhusiano huu na hivyo tofauti na mifanano kati ya spishi na vikundi vya spishi.<ref>{{cite book | last = Neill | first = Campbell | authorlink = | title = Biology; Fourth edition | publisher = [[The Benjamin/Cummings Publishing Company]] | series = | year = 1996 | doi = | isbn = 0-8053-1940-9 | page = G-21 (Glossary)}}</ref> Hata hivyo, utafiti wa mifumo ulikuwa uga hai wa utafiti muda mrefu kabla ya mawazo ya mageuko hayajakuwa ya kawaida.<ref>{{cite book | last = Douglas | first = Futuyma | authorlink = | title = Evolutionary Biology; Third edition | publisher = [[Sinauer Associates]] | series = | year = 1998 | doi = | isbn = 0-87893-189-9 | page = 88}}</ref> Uainishaji, taksonomia, na utaratibu wa majina wa viumbehai vya biolojia unasimamiwa na Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya Kizoolojia, Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya Kibotania, na Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya Bakteria kwa wanyama, mimea, na bakteria, mtawalia. Uanishaji wa virusi, viroidi, prioni, na ajenti wengine wote wadogo wa virusi wanaoonyesha sifa bainifu za kibiolojia unafanywa na Kanuni ya Kimataifa ya Uainishaji na Utaratibu wa majina ya Virusi.<ref>[91] ^ [http://www.ictvonline.org/virusTaxonomy.asp Taksonomia ya Virusi ya ICTV 2009]</ref><ref>[92] ^ [http://www.ncbi.nlm.nih.gov/ICTVdb/Ictv/fs_pospi.htm "80.001 Popsiviroidae - ICTVdB Kielezo cha Virusi."] (Tovuti.) Tovuti ya Mashirika ya Afya ya Marekani. Ilirejeshwa tarehe 28-10-2009.</ref><ref> [http://www.ncbi.nlm.nih.gov/ICTVdb/Ictv/fs_prion.htm "90.][http://www.ncbi.nlm.nih.gov/ICTVdb/Ictv/fs_prion.htm Prions - ICTVdB Kielezo cha Virusi. "] (Tovuti.) Tovuti ya Mashirika ya Afya ya Marekani. Ilirejeshwa tarehe 28-10-2009.</ref><ref> [http://www.ncbi.nlm.nih.gov/ICTVdb/Ictv/fs_satel.htm "81.][http://www.ncbi.nlm.nih.gov/ICTVdb/Ictv/fs_satel.htm Satelaiti - ICTVdB Kielezo cha Virusi. "] (Tovuti.) Tovuti ya Mashirika ya Afya ya Marekani. Ilirejeshwa tarehe 28-10-2009.</ref> Hata hivyo, mifumo mingine kadhaa ya uainishaji wa virusi ipo. Kimapokeo, viumbe hai vimegawanywa katika jamii tano: Monera; Protista; Fungi; Plantae; Animalia.<ref>{{cite book|last=Margulis|first=L|coauthors=Schwartz, KV|authorlink=Lynn Margulis|title=Five Kingdoms: An Illustrated Guide to the Phyla of Life on Earth|edition=3rd|publisher= WH Freeman & Co|location=|year=1997|isbn=978-0716731832|series=|oclc=223623098 237138975}}</ref> Hata hivyo, wanasayansi wengi sasa wanafikiria kuwa mfumo huu wa jamii tano umepitwa na wakati. Mifumo mbadala ya kisasa ya uainishaji kwa jumla huanza na mfumo wa miliki tatu: Akea (awali Akeabakteria); Bakteria (awali yukabakteria); Yukariyota (ikiwa ni pamoja na protisti, kuvu, mimea, na wanyama)<ref name="domain">{{cite journal | author = Woese C, Kandler O, Wheelis M | title = Towards a natural system of organisms: proposal for the domains Archaea, Bacteria, and Eukarya | url=http://www.pnas.org/cgi/reprint/87/12/4576 | journal = Proc Natl Acad Sci USA | volume = 87 | issue = 12 | pages = 4576–9 | year = 1990 | pmid = 2112744 | doi = 10.1073/pnas.87.12.4576 | pmc = 54159 | ref = harv}}</ref> Miliki hizi huakisi kama seli zina viini au la, pamoja na tofauti katika vijenzi vya kemikali vya nje ya seli.<ref name="domain"/> Aidha, kila jamii inavunjwa mara kwa mara hadi kila spishi tofauti inaainishwa mbali mbali. Utaratibu ni: Miliki, Jamii; Ukoo, Kategoria, Aina, Familia, Jenasi; Spishi. Pia kuna mfululizo wa vimelea vya ndani ya seli vilivyo kwenye "ukingo wa maisha"<ref>[100] ^ Rybicki Ep (1990) "Uainisho ya viumbe katika makali ya maisha, au matatizo ya utaratibu wa virusi." ''S Aft J Sci'' 86:182-186</ref> katika shughuli za metaboli, kumaanisha kuwa wanasayansi wengi hawaainishi miundo hii kama hai, kutokana na ukosefu wao wa moja au zaidi ya kazi za msingi ambazo huelezea sifa bainifu za maisha. Vinaainishwa kama virusi, viroidi, prioni, au setilaiti. Jina la kisayansi la kiumbehai linatoka kwenye jenasi na spishi yake. Kwa mfano, binadamu wataorodheshwa kama Homo sapiens. Homo itakuwa jenasi na sapiens ni spishi. Unapoandika jina la kisayansi la kiumbehai, ni sahihi kuandika herufi ya kwanza katika jenasi kwa herufi kubwa na kuandika spishi zote kwa herufi ndogo. Zaidi ya hayo, neno lote litapigwa chapa kwa herufi mlazo au litapigwa mstari.<ref>{{cite book | url = http://books.google.com/?id=hVUU7Gq8QskC&lpg=PA198&dq=species%20epithet%20capitalize&pg=PA198#v=onepage&q=species%20epithet%20capitalize | pages = 198 | title = Writing for Science and Engineering: Papers, Presentation | author = Heather Silyn-Roberts | year = 2000 | isbn = 0750646365 | publisher = Butterworth-Heinemann | location = Oxford}}</ref><ref>{{cite web | url = http://ibot.sav.sk/icbn/frameset/0065Ch7OaGoNSec1a60.htm#recF | title = Recommendation 60F | work = [[International Code of Botanical Nomenclature]], Vienna Code | year = 2006 | pages = 60F.1}}</ref> Mfumo wa kutawala wa uainishaji unaitwa taksonomia ya Linnaean, ambayo ni pamoja na vyeo na utaratibu wa majina wa vipeo. Jinsi ya kupatia viumbehai majina inadhibitiwa na mikataba ya kimataifa kama vile Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya kibotaniki (ICBN), Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya Kizoolojia (ICZN), na Kanuni ya Kimataifa ya Utaratibu wa majina ya Bakteria (ICNB). Rasimu unganishi, BioCode, ilichapishwa mwaka wa kusanifisha utaratibu wa majina katika maeneo haya matatu, lakini bado haijakubaliwa rasmi.<ref>{{cite conference | title=The BioCode: Integrated biological nomenclature for the 21st century? | booktitle=Proceedings of a Mini-Symposium on Biological Nomenclature in the 21st Century | author=John McNeill | date=1996-11-04}}</ref> Rasimu ya BioCode imepokea usikivu mdogo tangu mwaka wa 1997; tarehe yake ya utekelezaji iliyopangwa awali ya 1 Januari 2000, imepita bila kutambuliwa. Hata hivyo, jarida la mwaka wa 2004 juu ya sianobakteria linatetea kukubaliwa kwa Kanuni za Biolojia na hatua za muda zinazojumuisha kupunguza tofauti baina ya kanuni.<ref name="oren"> {{cite journal |author=Ahoren Oren |year=2004 |title=A proposal for further integration of the cyanobacteria under the Bacteriological Code |journal=Int. J. Syst. Evol. Microbiol. |volume=54 |pages=1895–1902 |doi=10.1099/ijs.0.03008-0 |pmid=15388760 |issue=Pt 5 |ref=harv }}</ref> Kanuni ya Kimataifa ya Uainishaji na Utaratibu wa majina ya Virusi (ICVCN) bado haijajumuishwa ndani ya Kanuni za Biolojia.

  Ikolojia

  Mfano kati ya samaki: shininewi (Amphiprion ocellaris) wanaoishi kati ya minyiri ya anemoni wa bahari wa tropiki. Samaki wa eneo hulinda anemoni kutoka kwa samaki wanaokula anemoni, na kwa upande mwingine minyiri yenye ukali ya anemoni hulinda shininewi kutoka kwa wawindaji wake
  Ikolojia inachunguza usambazaji na wingi wa viumbehai, na uhusiano kati ya viumbehai na mazingira yao.<ref>{{cite book |last=Begon |first=M. |coauthors= Townsend, C. R., Harper, J. L. |title=Ecology: From individuals to ecosystems. (4th ed.) |year=2006 |publisher=Blackwell |isbn=1405111178 }}</ref> Makazi ya kiumbehai na yanaweza kuelezwa kama sababu za vitu visivyo hai za mahali maalum kama vile hali ya hewa na ikolojia, pamoja na viumbehai vingine na sababu za vitu hai vinavyoshiriki mazingira yake.<ref name="habitats_of_the_world">{{Cite book | title = Habitats of the world | year = 2004 | url = http://books.google.com/?id=U-_mlcy8rGgC&pg=PA238 | publisher = Marshall Cavendish | location = New York | isbn = 978-0-7614-7523-1 | pages = 238 }}</ref> Sababu moja kwamba mifumo ya kibiolojia inaweza kuwa migumu kuchunguza ni kwamba uhusiano mwingi na viumbehai wengine na mazingira yanawezekana, hata kwa mizani midogo kabisa. Bakteria ya hadubini inayovutika kwa mwinamo wa sukari wa karibu inavutika kwa mazingira yake kama vile simba anavutika kwa mazingira yake wakati anapotafuta chakula katika savana ya Afrika. Kwa spishi ya aina yoyote, tabia zinaweza kuwa za ushirika, uchokozi, unyonyaji, au za kutegemeana. Mambo huwa magumu zaidi wakati spishi mbili au zaidi tofauti huathiriana katika mfumo wa ikolojia. Utafiti wa aina hii uko ndani ya taaluma ya ikolojia. Mifumo ya ikolojia huchunguzwa katika ngazi kadhaa tofauti, kutoka kwa watu binafsi na idadi ya watu hadi mifumo ikolojia na bayongahewa. Neno biolojia ya idadi mara nyingi hutumika kwa kubadilishana na ikolojia ya idadi, ingawa biolojia ya idadi mara nyingi zaidi hutumika wakati wa kuchunguza maradhi, virusi, na vijiumbe maradhi, ilhali ikolojia ya idadi kwa kawaida hutumiwa wakati wa kuchunguza mimea na wanyama. Kama inavyoweza kukisiwa, ikolojia ni sayansi inayotumia taaluma kadhaa. Etholojia huchunguza tabia ya wanyama (hasa ile ya wanyama wa kijamii kama vile mamalia wa hali ya juu na kanidi), na wakati mwingine inazingatiwa kama tawi la zoolojia. Wana etholojia wamejishughulisha na mageuko ya tabia na ufahamu wa tabia katika misingi ya nadharia ya uteuzi asilia. Kwa maana nyingine, mwana etholojia wa kwanza wa kisasa alikuwa Charles Darwin, ambaye kitabu chake, Kudhihirisha Hisia za Mtu na Wanyama, kiliwavutiwa wana etholoja wengi waliofuata.<ref name="black">{{Cite journal | pmc = 1279921 | pmid = 12042386 | year = 2002 | month = Jun | author = Black, J | title = Darwin in the world of emotions | volume = 95 | issue = 6 | pages = 311–3 | issn = 0141-0768 | journal = Journal of the Royal Society of Medicine | url = http://www.jrsm.org/cgi/pmidlookup?view=long&pmid=12042386 | format = Free full text | doi = 10.1258/jrsm.95.6.311 | ref = harv }}</ref> Biojiografia huchunguza usambazaji wa kuhusiana na anga wa viumbehai Duniani,<ref> Wiley, 1981</ref> ikilenga mada kama tectonics za sahani, mabadiliko ya hali ya hewa, kusambaa na uhamiaji, na kladistiki.

  Matawi ya biolojia

  Haya ni matawi muhimu ya biolojia:<ref>[118] ^ [http://www.biology-online.org/dictionary/Branches_of_biology Matawi ya Biolojia katika baiolojia-online.org]</ref><ref> Biolojia katika bellaonline.com

Marejeo

Viungo vya nje

Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
biolojia
Viungo vya majarida
This article is issued from Wikipedia - version of the 4/20/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.