Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz

Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz
Yıldız Teknik Üniversitesi
Walimu 1384
Wanafunzi 21,000
Mahali {{{mji}}}

Yıldız Teknik Üniversitesi (YTÜ, au YTU kwa lugha ya KiingerezaChuo Kikuu cha ufundi cha Yildiz) ni chuo kikuu cha kiufundi, wakfu ya sayansi na uhandisi na ni moja ya taasisi za elimu maarufu zaidi katika mji wa Istanbul, Uturuki. Chuo hii ipo ndani ya wilaya Beşiktaş.

Historia

YTU kuu ya jengo.

Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz kilianza 1911. YTU ilianzishwa kama Kondüktör Mekteb-i Âlisi / Shule ya Elimu ya Juu ili kuweza kukabiliana na mahitaji ya Manispaa ya Umma na Sehemu ya Kazi na kutoa huduma kwa "afisa wa sayansi" (waliojulikana awali kama conductors, na leo kama mafundi). Shule hiyo iliundwa ili ufwate mfumo wa elimu ya juu ya ufundi ya "École de Conducteur" na iliungwa na Wizara ya Kazi za Umma.

Jina la shule lilibadilishwa na kuitwa Nafia Fen Mektebi mwaka 1922 na muda wa elimu uliongezwa kutoka miaka 2,5 hadi miaka 3 kati ya mwaka 1926 na 1931.

Kufuatia kuongezeka kwa huduma za umma na mahitaji ya huduma za kiufundi, sheria mpya iliamuru kufungwa kwa Nafia Fen Mektebi na kuanzishwa kwa shule ya Ufundi ili kukabiliana na pengo lililokuwa kati ya maafisa wa kiufundi na wahandisi wa kitaaluma. shule hiyo ilikuwa na mpango wa miaka 2 kwa ajili ya maafisa wa kiufundi na mpango wa miaka 4 kwa ajili ya uhandisi na ulipewa baadhi ya majengo ya ukumbi wa Yildiz, ambayo bado yako katika matumizi hadi leo.

Katika vipindi vya mwanzo shule ilitoa elimu ya ujenzi na idara za mitambo ya sayansi ili kuelimisha wanafunzi kuwa walinzi wa kiufundi na wahandisi. Kati ya 1942-1943 idara ya usanifu na ya umeme zilianzishwa kama sehemu ya idara ya uhandisi. shule hiyo ilikubaliwa kama moja ya vyuo vya elimu ya juu na taasisi ya utafiti katika mwaka 1969. Mwaka 1971 sheria mpya ilitoa amri ya kufungwa kwa shule maalum za ufundi, vyuo vya uhandisi viliimarishwa na Jimbo la Uhandisi na chuo cha kimimari cha Istanbul.

Yildiz teknik Üniversitesi ilikubaliwa kama jina rasmi la shule mwaka 1992. Kitivo cha Uhandisi kiligawanywa katika vyuo vinne, Kitivo cha umeme, Kitivo cha Ujenzi, Kitivo cha Mitambo na Vyuma na Kitivo cha Sayansi ya Uchumi na Utawala. Kitivo cha Uhandisi cha Kocaeli na Shule ya Ufundi ya Kocaeli vilitengwa na chuo kikuu cha Yildiz na kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kocaeli. Leo YTU inatoa elimu katika vyuo vyake 9, taasisi 2, Shule ya Ufundi ya Elimu ya Juu na Shule ya Mafunzo ya Lugha za Nje kwa zaidi ya wanafunzi 17.000.

Vitivo

Galeri

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz

Kigezo:Vyuo vya ufundi Uturuki Kigezo:Vyuo vikuu ıstanbul Kigezo:Vyuo vikuu Uturuki Anwani ya kijiografia: 41°03′05″N 29°00′43″E / 41.05149°N 29.01191°E / 41.05149; 29.01191

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/27/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.