Eneo

Maumbo matatu ya jiometria yenye maeneo tofauti (msambamba, pembetatu, duara)

Eneo katika elimu ya jiometria ni idadi inayoeleza ukubwa wa umbo bapa lenye upana na urefu. Kwa hiyo „eneo“ linataja ukubwa wa gimba lenye wanda mbili.

Hii inamaanisha maumbo ya jiografia bapa kama vile mraba, mstatili na duara lakini pia uso wa gimba lenye wanda tatu kama vile mchamrembe au tufe.

Ukubwa wa eneo linapimwa kwa kuulinganisha na miraba maalumu. Katika mfumo wa vipimo sanifu vya kimataifa kizio sanifu ni mita ya mraba (inayofupishwa kwa m²). Umbo kama mviringo mwenye eneo la 3 una eneo sawa na miraba mitatu ya aina hii.

Matumizi ya kipimo cha eneo

Makadirio ya eneo yana faida nyingi katika maisha ya kila siku. Nikitaka kupiga rangi kuta za chumba naweza kupima maeneo yote ya kuta zake. Kwa mfano chumba cha mita 3x4 na kimo cha mita 2 lina eneo la kuta zake za 28 m² (Kuta 2 zenye upana wa mita 3 x kimo mita 2 ni 2x3=6 x kimo 2 = 12m²; kuta 2 zenye upana wa mita 4 ni 2x4= 8 x kimo 2= 16 m²; 16m²+18m² = 28 m²). Nikijua hii naweza kuuliza dukani je wana rangi gani kwa ajili ya ukuta na kopo la rangi linatosha kwa mita za mraba ngapi? Wakisema 10 m ² najua nitahitaji kununua kopo 3. Katika mfano wa juu naweza kutoa eneo la mlango na madirisha labda zinatosha kopo 2 kubwa na 1 ndogo.

Vivyo hivyo naweza kukadiria kiasi cha mbolea kwa eneo la shamba na kadhalika.

Tetrahedroni
Pia ambako uso umetandazwa bapa

Makadirio ya eneo la umbo

Umbo Majina Eneo A
Mraba Urefu wa upande a A = a^2
Mstatili Urefu wa pande a,\,b A = a \cdot b
Pembetatu
Upande wa msingi g, kimo h, pembemraba kwa g A = \frac{g \cdot h}{2}
Duara Rediasi r A = \pi r^2

Makadirio ya eneo la uso la gimba

Gimba Majina Eneo la uso A
Mchemraba Urefu wa upande a A = 6a^2
Tetrahedroni Urefu wa upande a A = \sqrt{3}\,a^2
Tufe
Rediasi r A = 4\pi r^2
Pia Rediasi ya duara la msingi r, Kimo h A = \pi r (r + \sqrt{r^2+h^2})
This article is issued from Wikipedia - version of the 4/10/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.