Jibuti

Ramani ya Jibuti
جمهورية جيبوتي
Ǧumhūriyyah Ǧībūtī
République de Djibouti

Jamhuri ya Jibuti
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Jibuti tumeichagua
Wimbo wa taifa: {{{national_anthem}}}
Mji mkuu Jibuti
11°36 N 43°10 E
Mji mkubwa nchini Jibuti
Lugha rasmi Kiarabu na Kifaransa
Serikali
Rais
Jamhuri
Ismaïl Omar Guelleh
Uhuru
Tarehe
27 Juni 1977
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
23,200 km² (ya 150)
0.09% (20 km² / 7.7 mi²)
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
810,179 (ya 168)
460,700
37.2/km² (ya 154)
Fedha Franc (DJF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
+3 (UTC)
Intaneti TLD .dj
Kodi ya simu +253

-

Jibuti (kwa Kifaransa Djibouti, kwa Kiarabu: جيبوتي) ni nchi ndogo ya Afrika ya Mashariki kwenye Pembe la Afrika.

Imepakana na Eritrea, Ethiopia na Somalia upande wa bara. Kuna pwani ya Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden. Ng'ambo ya bahari iko nchi ya Yemen katika umbali wa km 20 pekee.

Jina la nchi linatokana na lile la mji mkuu, Jibuti.

Historia

Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Somalia ya Kifaransa, halafu (1967) Eneo la Kifaransa la Waafar na la Waisa, kutokana na majina ya makabila mawili makubwa zaidi ya eneo hilo.

Sababu ya kuanzishwa kwa koloni ilikuwa nia ya Ufaransa ya kuwa na bandari ya mji wa Jibuti karibu na Bab el Mandeb inayotawala mawasiliano kati ya Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kuelekea Mfereji wa Suez.

Nchi ilipata uhuru tarehe 27 Juni 1977.

Watu

Siku hizi wakazi wengi (60%) ni Wasomali, hasa wa kabila la Waisa, halafu Waafar (35%). Asilimia 5 zilizobaki ni Waarabu, Waethiopia na Wazungu (hasa Wafaransa na Waitalia).

Lugha rasmi ni Kifaransa na Kiarabu. Kisomali ni Kiafar ni lugha za taifa.

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 94% za wakazi na ndio dini rasmi pekee. Asilimia 6 wanafuata Ukristo katika madhehebu mbalimbali, hasa Waorthodoksi wa Mashariki kutoka Ethiopia (3.2%), halafu Wakatoliki (1.4%) na Waprotestanti (chini ya 1%).

Viungo vya nje

Serikali
Taarifa za jumla
Mengineyo


Nchi za Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jibuti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 9/30/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.