Kalenda ya Kiislamu

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Historia ya Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Nguzo za Kiislamu
Shahada Swala Saumu
Hija Zaka

Watu muhimu

Muhammad

Abu Bakr Ali
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'an Sunnah Hadithi
Sheria Kalam
Wasifu wa Muhammad
Sharia

Aina za Uislamu

Sunni Shi'a Kharijite

Tamaduni za Kiislamu

Shule Historia
Tauhidi Falsafa Sayansi
Sanaa Ujenzi Miji
Kalenda Sikukuu
Wanawake
Viongozi Siasa
Umma Itikadi mpya Sufii

Tazama pia

Kamusi Kuogopa Uislamu

Kalenda ya Kiislamu ni mtindo wa kuratibu wakati unaopatikana katika nchi mbalimbali za Kiislamu.

Pia Waislamu wanaoishi katika mazingira yasiyo ya Kiislamu hutumia kalenda hii kwa ajili ya kupanga maisha yao ya kidini, hasa sikukuu na saumu.

Mahali pengi Kalenda ya Kiislamu hutumika pamoja na kalenda zinazofuata mwendo wa jua, hasa kalenda ya Kikristo ambayo ndiyo iliyoenea zaidi duniani.

Miezi na mwaka

Kalenda ya Kiislamu imepokea kawaida ya mwaka wa Waarabu wa kale: mwaka una miezi 12.

"Mwezi" humaanisha kipindi kamili kati ya kuonekana kwa mwezi angani mara ya kwanza (hilal) hadi kurudia kwa kuonekana kwake. Kwa sababu muda wa kipindi hiki ni siku 29,5 mwezi halali huhesabiwa kuwa na siku 29 au 30. Kipindi kinachoitwa "mwezi" katika kalenda ya Kikristo hakina uhusiano tena na mwezi halisi.

Waislamu wanaofuata mfano wa Kisaudi hukubali mwezi mpya umeanza kama umeonekana kwa macho. Kwa sababu desturi hii imeleta matatizo ya kutokubaliana, pia ni rahisi kukadiria mwendo wa mwezi, nchi mbalimbali za Kiislamu hutumia makadirio ya kitaalamu kupanga tarehe za miezi.

Idadi ya siku katika mwaka wa Kiislamu ni 354.

Hesabu ya miaka

Taz. makala "Miaka baada ya hijra"

Hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiislamu hufuta utaratibu wa "miaka baada ya hijra" yaani tangu kuhamia kwake Mtume Muhammad kutoka Makka kwenda Madina. Hijra ilitokea mwaka 622 BK au katika mwaka 1 wa hesabu yenyewe.

Njia inayofuata inasaidia kujua takriban tarehe gani ya Kiislamu inalingana na tarehe ipi katika kalenda ya Kikristo:

K (Mwaka "baada ya Kristo" katika kalenda ya Kikristo), H (Mwaka "Baada ya Hijra" katika kalenda ya Kiislamu)

Kati ya nchi za Kiislamu Uajemi na Afghanistan hutumia mwaka wa jua wakihesabu tangu hijra. Lakini pamoja na kalenda hii wanatumia mwaka wa kimwezi wa Kiislamu kwa kupanga sikukuu za dini.

Miezi

Miezi yenye sikukuu muhimu ni hasa

Mwezi wa Muharram ni muhimu sana kati ya Washia wanaokumbuka mateso na kifo cha Imam Husain wakati wa mapigano ya Karbala.

Majina na mfuatano wa miezi ni hivi:

 1. Muharram محرّم
 2. Safar صفر
 3. Rabi`-ul-Awwal (Rabi' I) ربيع الأول
 4. Rabi`-ul-Akhir (Rabi' II) ربيع الآخر أو ربيع الثاني
 5. Jumaada-ul-Awwal (Jumaada I) جمادى الأول
 6. Jumaada-ul-Akhir (Jumaada II) (Jumaada II) جمادى الآخر أو جمادى الثاني
 7. Rajab رجب
 8. Shaaban شعبان
 9. Ramadan رمضان
 10. Shawwal شوّال
 11. Dhul Qaadah ذو القعدة
 12. Dhul Hijjah ذو الحجة

Siku za Juma au Wiki

Kalenda ya Kiislamu hutumia juma au wiki ya siku saba jinsi ilivyo kawaida kwa Wayahudi na Wakristo. Siku muhimu zaidi ni Ijumaa ambako Waislamu hukusanyika kwa ajili ya sala ya pamoja.

Kwa Kiarabu majina ya siku za juma hufuata hesabu ya Kiyahudi jinsi inavyoonekana katika Biblia. Jumapili inaitwa "siku ya kwanza", Jumatatu "siku ya pili" hadi "siku ya tano" = Alhamisi. Siku ya sita pekee imepewa jina jipya la Kiislamu kutokana na mkutano wa sala ya pamoja.

Siku ya saba tena imebaki na jina lake la Kibiblia "Sabato" au siku ya saba. Hii ni kwa sababu utamaduni wa Kiarabu kabla ya Uislamu uliwahi kupokea athira nyingi kutoka kwa Wayahudi na Wakristo, pia walikuwepo Waarabu ambao upande wa dini walikuwa Wakristo na Wayahudi.

Majina ya siku katika lugha ya Kiswahili yanaonyesha ya kwamba lugha ilianza katika mazingira ya Kiislamu kabisa, bila athira za moja kwa moja kutoka Uyahudi au Ukristo. Majina ya siku yamepangwa kufuatana na Ijumaa ambayo ni siku muhimu hasa katika maisha ya Kiislamu. Maana ya Jumamosi, Jumapili n.k. ni "Siku ya kwanza, pili, tatu" baada ya Ijumaa. Alhamisi imebaki na jina la Kiarabu.

Jumapili: yaum al-ahad (siku ya kwanza) يوم الأحد
Jumatatu: yaum al-ithnayna (siku ya pili) يوم الإثنين
Jumanne: yaum ath-thalatha (siku ya tatu) يوم الثلاثاء
Jumatano: yaum al-arba`a (siku ya nne) يوم الأَربعاء
Alhamisi: yaum al-khamis (siku ya tano) يوم خميس
Ijumaa: yaum al-jum`a (siku ya mkutano) يوم الجمعة
Jumamosi: yaum as-sabt (siku ya sabato) يوم السبت
This article is issued from Wikipedia - version of the 9/12/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.