Kazakhstan

Қазақстан Республикасы
Qazaqstan Respublïkası
Республика Казахстан
Respublika Kazakhstan

Jamhuri ya Kazakhstan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Kazakhstan yangu
Mji mkuu Astana
51°10 N 71°30 E
Mji mkubwa nchini Almaty
Lugha rasmi Kikazakh, Kirusi
Serikali
Rais
Waziri Mkuu
Jamhuri
Nursultan Nazarbayev
Karim Massimov
Uhuru
Ilitangazwa
ilikamilika

16 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,724,900 km² (ya 9)
1.7
Idadi ya watu
 - July 2015 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
17,563,300[1] (ya 62)
14,953,100
5.94/km² (ya 227)
Fedha Tenge ya Kazakhstan (KZT)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+5 to +6)
(UTC)
Intaneti TLD .kz
Kodi ya simu +7

-

Ramani ya Kazakhstan

Kazakhstan (pia: Kazakistan) ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa iko katika Asia ya Kati.

Imepakana na Urusi, China, Kyrgyzstan, Uzbekistan na Turkmenistan.

Mji mkuu ni Astana; Almaty ilishika nafasi hiyo hadi 1996.

Jiografia

Kazakhstan ina eneo la km² 2,717,300; ni nchi kubwa ya tisa duniani. Sehemu kubwa iko upande wa Asia na nyingine ndogo upande wa Ulaya.

Upande wa magharibi inaanza katika tambarare za mto Volga pamoja na Bahari ya Kaspi na kuelekea hadi milima ya Altai upande wa China. Kusini iko milima ya Tienshan yenye kimo cha mita 7,000 na ziwa Aral. Upande wa kaskazini hakuna mpaka asilia na Siberia.

Historia

Hadi mwaka 1991 ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikazakhi".

Wakazi

Wakazi wengi (63.6%) ni Wakazaki wanaozungumza lugha ya jamii ya Kituruki, wakifuatwa na Warusi wanaozungumza lugha yao ya jamii ya Kislavoni (23.3%). Ya kwanza ndiyo lugha ya taifa, ya pili ni pia lugha rasmi. Kuna makabila mengine 30, kama vile Wauzbeki (2.8%), Waukraina (2.1%) n.k.

Upande wa dini, 70.2% ni Waislamu (hasa Wasuni) na 26.2% Wakristo (hasa Waorthodoksi 23.9%, wakifuatwa na Wakatoliki na Waprotestanti, jumla 2.3%). Baada ya uhuru, dini zote zimepata uhai mpya na kujenga maabadi mengi. Serikali haina dini, lakini inaziheshimu zote.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

 • Alexandrov, Mikhail (1999). Uneasy Alliance: Relations Between Russia and Kazakhstan in the Post-Soviet Era, 1992–1997. Westport, CT: Greenwood Press. ISBN 0-313-30965-5. 
 • Clammer, Paul (2004). Lonely Planet Guide: Central Asia. Oakland, CA: Lonely Planet. ISBN 1-86450-296-7. 
 • Cummings, Sally (2002). Kazakhstan: Power and the Elite. London: Tauris. ISBN 1-86064-854-1. 
 • Demko, George (1997). The Russian Colonization of Kazakhstan. New York: Routledge. ISBN 0-7007-0380-2. 
 • Fergus, Michael (2003). Kazakhstan: Coming of Age. London: Stacey International. ISBN 1-900988-61-5. 
 • George, Alexandra (2001). Journey into Kazakhstan: The True Face of the Nazarbayev Regime. Lanham: University Press of America. ISBN 0-7618-1964-9. 
 • Martin, Virginia (2000). Law and Custom in the Steppe. Richmond: Curzon. ISBN 0-7007-1405-7. 
 • Nazarbayev, Nursultan (2001). Epicenter of Peace. Hollis, NH: Puritan Press. ISBN 1-884186-13-0. 
 • Nazpary, Joma (2002). Post-Soviet Chaos: Violence and Dispossession in Kazakhstan. London: Pluto Press. ISBN 0-7453-1503-8. 
 • Olcott, Martha Brill (2002). Kazakhstan: Unfulfilled Promise. Washington, DC: Brookings Institution Press. ISBN 0-87003-189-9. 
 • Rall, Ted (2006). Silk Road to Ruin: Is Central Asia the New Middle East?. New York: NBM. ISBN 1-56163-454-9. 
 • Robbins, Christopher (2007). In Search of Kazakhstan: The Land That Disappeared. London: Profile Books. ISBN 978-1-86197-868-4. 
 • Rosten, Keith (2005). Once in Kazakhstan: The Snow Leopard Emerges. New York: iUniverse. ISBN 0-595-32782-6. 
 • Thubron, Colin (1994). The Lost Heart of Asia. New York: HarperCollins. ISBN 0-06-018226-1. 

Viungo vya nje

Serikali

Biashara

Anwani ya kijiografia: 48°N 68°E / 48°N 68°E / 48; 68

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kazakhstan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kazakhstan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 12/6/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.