Kigiriki

Alfabeti ya Kigiriki
Α α Alfa Β β Beta
Γ γ Gamma Δ δ Delta
Ε ε Epsilon Ζ ζ Dzeta
Η η Eta Θ θ Theta
Ι ι Iota Κ κ Kappa
Λ λ Lambda Μ μ Mi
Ν ν Ni Ξ ξ Ksi
Ο ο Omikron Π π Pi
Ρ ρ Rho Σ σ Sigma
Τ τ Tau Υ υ Ipsilon
Φ φ Phi Χ χ Khi
Ψ ψ Psi Ω ω Omega

Kigiriki (pia: Kiyunani) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya inayotumiwa hasa nchini Ugiriki. Maandishi yake yamejulikana tangu miaka 3500. Hakuna lugha nyingine duniani inayozungumzwa hadi leo yenye historia ndefu kuliko hii, isipokuwa Kichina.

Kigiriki ni muhimu sana kwa utamaduni wa kisasa kwa sababu ya kutoa michango mingi kwa lugha ya sayansi, teknolojia na utamaduni. Fikra nyingi muhimu zilionekana mara ya kwanza kwa Kigiriki na falsafa iliyojadiliwa na kuandikwa kwa lugha hii.

Alfabeti ya Kigiriki ilikuwa msingi wa alfabeti mbili, za Kilatini na Kikirili, pia kwa miandiko ya abijadi kama herufi za Kiarabu au za Kiebrania. Kiswahili huandikwa kwa herufi za Kilatini.

Kati ya maandiko muhimu ya Kigiriki ni yale ya wanafalsafa kama Plato na Aristoteles na pia maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya pamoja na Deuterokanoni).

Kati ya karne ya 3 KK hadi karne ya 6 BK Kigiriki kilikuwa lugha ya kimataifa katika eneo kubwa la kandokando ya bahari ya Mediteranea pamoja na Mashariki ya Kati.

Lugha imeendelea kubadilika kisarufi na pia kimsamiati. Hivyo Kigiriki cha kale kimekwisha, hakizungumzwi tena na watu, lakini bado kinafundishwa.

Leo hii katika nchi ya Ugiriki kuna lugha ya Kigiriki Kipya kinachoendela kuandikwa kwa herufi zilezile.

Ulingano wa Kigiriki cha Kale na cha Kisasa

Kigiriki cha Kisasa Kigiriki cha Kale
1 Στην αρχή ήταν ο Λόγος, και ο Λόγος ήταν προς τον Θεό(ν), και Θεός ήταν ο Λόγος. 1 Ἐν ἀρχῇ ἦν ὁ Λόγος, καὶ ὁ Λόγος ἦν πρὸς τὸν Θεόν, καὶ Θεὸς ἦν ὁ Λόγος.
/stin ar'khi 'itan o 'logos ke o 'logos 'itan pros ton thi'o ke thi'os 'itan o 'logos/ /en ar'khe en o logos kaí o lógos en prós tón the'on kaí the'os en o lógos/
Kwa Kiswahili: Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. (Injili ya Yohane, 1,1)

Viungo vya nje

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/22/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.