Kitabu cha Mika

Kitabu cha Mika ni kimoja kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh.

Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi na muda

Jina la nabii huyo, aliyefanya kazi wakati uleule wa nabii Isaya, mwishoni mwa karne ya 8 K.K., lina maana ya "Nani kama Mungu?".

Muhtasari

Kitabu kinaweza kuwaganyika sehemu nne ambamo vitisho na ahadi vinapokezana:

Dondoo maarufu

Tunavyosoma katika Injili ya Mathayo (2:1-6), dondoo la Mik 5:2 lilitumiwa na Wayahudi kutarajia ujio wa Masiya wa ukoo wa Mfalme Daudi kutoka Bethlehemu.

Dondoo lenyewe lilibainisha miaka 700 kabla ya Yesu kuzaliwa kwamba Bethlehemu hiyo ni ile ya Efrata, si nyingine yenye jina hilohilo: "Bali wewe, Betlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele".

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Kitabu cha Mika
This article is issued from Wikipedia - version of the 4/22/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.