Kitabu cha Yoshua bin Sira

Kitabu cha Yoshua bin Sira ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 K.K. - 175 K.K. huko Aleksandria (Misri).

Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji.

Ingawa kitabu hakionyeshi mpangilio mzuri, kwa kugusagusa mambo mbalimbali, mafundisho yake makuu ni kwamba Hekima, ambayo ni mamoja na Torati, ni sifa maalumu ya Wayahudi; hao tu wanaweza kumfikia Mungu.

Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

This article is issued from Wikipedia - version of the 3/9/2013. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.