Lugha rasmi

Ancient Tamil inscription at the Brihadeeswara Temple in Thanjavur

Lugha rasmi ni lugha iliyopewa cheo maalumu katika nchi fulani. Kwa kawaida ni lugha inayotumiwa hasa na serikali kwa mawasiliano kati ya ofisi zake na pia kwa matangazo rasmi kwa mfano kwa kutangaza sheria. Ni pia lugha ya kuendesha kesi mahakamani na kuandika hukumu.

Kuna nchi penye lugha rasmi moja tu lakini nchi nyingi huwa na lugha mbalimbali zinazokubaliwa kama lugha rasmi kwenye ngazi tofauti za serikali.

Katika nchi mbalimbali lugha rasmi imetajwa katika katiba ya taifa au katika sheria mahsus. Lakini nchi nyingine hazina sheria juu ya lugha rasmi hata kama hali halisi ipo na kueleweka.

Kwa mfano nchini Namibia Kiingereza ni lugha rasmi kufuatana na katiba lakini lugha 11 nyingine (pamoja na Kiafrikaans na Kijerumani) zimetajwa kama lugha za kitaifa zinazoweza kutumiwa pia kama lugha ya mafundisho shuleni.

Nchi kadhaa zimekubali pia lugha ya alama jinsi inavyotumiwa na watu bubu kati ya lugha rasmi ya nchi.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha rasmi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 6/30/2014. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.