Msumbiji

República de Moçambique
Jamhuri ya Msumbiji
Lugha ya taifa Kireno
Mji Mkuu Maputo
Aina ya Serikali Jamhuri
Rais Filipe Nyusi
Waziri Mkuu Carlos Agostinho do Rosário
Eneo km² 801.590
Wakazi 24,692,144 (Julai 2014)
Wakazi kwa km² 28.7
JPT/ Mkazi 233 US-$ (2004)
Uhuru kutoka Ureno tar. 25.06.1975
Pesa Metical (MZM)
Wakati UTC +2h
Wimbo wa Taifa Pátria Amada (kwa Kireno: Nchi pendwa)
Namba ya simu ya kimataifa +258

Msumbiji (kwa Kireno: Moçambique) ni nchi ya Afrika ya Kusini-Mashariki.

Msumbiji iko ufukoni mwa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Uswazi.

Upande wa mashariki kuna kisiwa cha Madagaska ng'ambo ya mlango bahari wa Msumbiji.

Jina la nchi limetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kwa Kireno: Ilha de Moçambique) kilichokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.

Sikukuu ya Taifa ni tarehe 25 Juni, ulipopatikana na uhuru mwaka 1975.

Jiografia

Ramani ya Msumbiji

Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, lakini kwenda kaskazini upana wake unapungua.

Nyuma ya tambarare nchi inapanda hadi kufika uwiano wa tambarare ya juu ya Afrika ya Kusini.

Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB: iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.

Mito iko mingi, mkubwa zaidi ukiwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani kwa Tanzania, Save na Limpopo.

Ziwa la Nyassa ni sehemu ya mpaka na Malawi.

Umbo la eneo la nchi ni refu sana: ni kilomita 2000 kutoka mpaka wa Tanzania upande wa kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini.

Pwani ya Bahari Hindi ina urefu wa km 2.470.

Miji mikubwa zaidi ni Maputo (wakazi 1.191.613), Matola (wakazi 543.907) na Beira (wakazi 530.706).

Historia

Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi ambao walimeza wakazi wa kwanza inavyothibitishwa na DNA.

Haijulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.

Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.

Taarifa za kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.

Baadaye Msumbiji ikawa koloni la Wareno hadi mwaka 1975 vita vya ukombozi vya miaka 1964-1974 vilipomalizika kwa ushindi.

Hata hivyo vilifuata vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 1977-1992.

Watu

Nchini Msumbiji kuna makabila mengi sana, kama vile Wamakua,Wanyungwe, Wayao, Wamakonde na Watsonga.

Kila kabila lina lugha yake, lakini lugha rasmi ni Kireno.

Upande wa dini, 56.1% ni Wakristo (hasa Wakatoliki, ambao ni 28.4%) na 17.9% ni Waislamu. 7.3% wanafuata dini asilia za Kiafrika au nyingine. Kumbe 18.7% hawana dini yoyote, kufuatana na kampeni ya Ukomunisti ya miaka 1979-1982.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Serikali
Habari
Taarifa za jumla
Asasi zisizolenga faida
Utalii
Afya


Nchi za Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msumbiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 10/4/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.