Namibia

Republic of Namibia
Jamhuri ya Namibia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unity, Liberty, Justice
Wimbo wa taifa: Namibia, Land of the Brave (Namibia, nchi ya mashujaa)
Mji mkuu Windhoek
22°33 S 17°15 E
Mji mkubwa nchini Windhoek
Lugha rasmi Kiingereza1
Serikali
Rais
Waziri Mkuu
Jamhuri
Hage Geingob
Saara Kuugongelwa
Uhuru
Kutoka Afrika Kusini
21 Machi 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
825,615 km² (ya 34)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,030,6922 (ya 147)
2,113,077
2.54/km² (ya 235)
Fedha Namibia dollar (NAD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+1)
(UTC)
Intaneti TLD .na
Kodi ya simu +264

-

Namibia ni nchi ya Afrika ya Kusini kwenye pwani ya Atlantiki.

Imepakana na Angola, Zambia, Zimbabwe Botswana na Afrika Kusini.

Imepata uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990.

Mji mkuu ni Windhoek (wakazi 322.500).

Jiografia

Sehemu kubwa ya nchi ni kavu sana na jangwa za Namib na Kalahari zinafunika asilimia kubwa ya uso wa nchi.

Jangwa la Namib liko upande wa magharibi likifuata pwani ya Atlantiki kuanzia Afrika Kusini hadi Angola. Upande wa mashariki kuna jangwa la Kalahari linalovuka mpaka wa Botswana.

Katikati ya majangwa hayo kuna nyanda za juu zinazofikia kimo cha mita 1700 kwa wastani.

Historia

Historia ya kale

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Chini ya ukoloni

Namibia katika mipaka ya sasa ilianzishwa katika karne ya 19 kama koloni la Ujerumani kwa jina la Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Uingereza na Afrika Kusini. Tangu mwaka 1919 ilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa chini ya serikali ya Afrika Kusini.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia serikali ya Afrika Kusini ilieneza siasa yake ya apartheid pia katika Afrika ya Kusini-Magharibi ikijaribu kulitendea eneo hilo kama sehemu kamili ya Afrika Kusini. Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingi za dunia.

Mwaka 1978 Umoja wa Mataifa uliamua ya kwamba Afrika ya Kusini-Magharibi unapaswa kupewa uhuru. Baada ya miaka ya vita vya kupigania uhuru kati ya SWAPO na jeshi la Afrika Kusini, mchakato wa kimataifa wa kuelekea uhuru ulianza mwaka 1988 na hatimaye mwaka 1990 nchi ilipata uhuru wake kwa jina la Namibia.

Watu

Wakazi wengi ni wa makabila ya Wabantu, hasa Waovambo (49.5%). Pia wako wengi wa jamii ya Khoisan, ambao wametokana na wenyeji wa nchi.

Asilimia 7 wana asili ya Ulaya, hasa Makaburu na Wajerumani, na asilimia 8 ni machotara.

Oshiwambo ni lugha ya kwanza ya karibu nusu ya wakazi, lakini Kiingereza ndicho lugha rasmi ingawa ni lugha ya kwanza ya 3% pekee za wakazi. (Angalia Orodha ya lugha za Namibia.)

11.3% za wakazi wanatumia lugha za Kikhoisan.

Kijerumani na Kiafrikaans zilikuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza hadi uhuru. Wakazi wengi hutumia Kiafrikaans kama lugha ya pili, na 10.4% kama lugha ya kwanza. Kijerumani ni lugha ya kwanza wa 32% za wakazi wenye asili ya Ulaya.

Kireno kinatumiwa na 4-5% za wakazi, hasa wenye asili ya Angola.

Upande wa dini, 80-90% za wakazi ni Wakristo (hasa Walutheri, Wakatoliki ni 13.7%). Waliobaki kwa kawaida wanafuata dini asilia za Kiafrika.

Picha za Namibia

Tazama pia

Viungo vya nje

Serikali
Elimu
Rushwa
Utalii
Kulinda amani


Nchi za Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Namibia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 1/7/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.