Hifadhi ya Ngorongoro

Makundi ya wanyamapori katika kasoko.
Ramani ya eneo.
Eneo la Ngorongoro lipo kaskazini mwa Tanzania.
Ndani ya kreta.

Ngorongoro ("Ngorongoro Conservation Area") ni eneo la kasoko kubwa nchini Tanzania, kwenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha; pia ni hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani. Eneo hili ni sehemu ya mbeya.

Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.

Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua.

Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita.

Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO upande wa uasilia.

Katika sekta ya utalii, ambayo nchi kama nchi huitegemea kwa kiasi fulani, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.

Picha

Kwa sababu ya aina mbalimbali za wanyama walioko, kreta ya Ngorongoro inafahamika kama kivutio cha utalii duniani.
Mandhari ya kreta ya Ngorongoro.

Tanbihi

  Marejeo

  Viungo vya nje

  Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Hifadhi ya Ngorongoro
  Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu.
  Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  This article is issued from Wikipedia - version of the 6/28/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.