Nyasi

Nyasi

Manyasi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Manyasi)
Ngazi za chini

Nusufamilia 12

 • Anomochlooideae
 • Aristidoideae
 • Arundinoideae
 • Bambusoideae
 • Centothecoideae
 • Chloridoideae
 • Danthonioideae
 • Ehrhartoideae
 • Panicoideae
 • Pharoideae
 • Pooideae
 • Puelioideae

Manyasi ni kundi la mimea inayofunika udongo; manyasi yaliyo mengi si kubwa sana lakini aina kama mianzi hufikia urefu wa miti. Kibiolojia hujumlishwa katika familia ya Poaceae au Gramineae.

Manyasi mengi huwa na mizizi mirefu inayoshika ganda la juu la ardhi hivyo kuzuia au kupunguza mmomonyoko wa udongo. Kiekolojia aina za manyasi zimezoea mazingira tofauti kabisa kati ya kanda za joto hadi kanda za baridi sana. Wakati wa baridi au ukame majani juu ya ardhi hukauka hata kupotea kabisa lakini mizizi ina uwezo kulala uda mrefu na kusubiri mvua au halijoto ya juu zaidi.

Lishe ya wanyama

Watu wametumia manyasi kwa shughuli mbalimbali. Nyasi ni muhimu kama lishe ya wanyama kama ng'ombe au kondoo. Wanyama wengi wa pori wanakula nyasi vilevile. Wakulima wanaweza kuteua aina za manyasi zinazofaa kama lishe ya mifugo na kuzipanda.

Nafaka

Aina kadhaa za manyasi hutoa mbegu zinazoliwa na watu kama nafaka; manyasi haya ya nafaka kama vile mahindi, mpunga au ngano ni kati ya vyakula vya kimsingi vya binadamu duniani.

Mimea kwa burudani

Katika mazingira ya mjini manyasi ya pekee hutumiwa kufunika ardhi hasa katika maeneo ya bustani za mjini yanayokanyagwa na watu wengi wanaopenda kukalia kwenye manyasi na kupumzika; aina hizi zinatumiwa pia kwenye viwanja vya michezo.

Majina ya aina za manyasi katika Afrika ya Mashariki

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/7/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.