Okapi

Okapi

Okapi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Mamalia - wanyama wanaonyonyesha watoto wao)
Oda: Artiodactyla (Mamalia wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili)
Familia: Giraffidae (Mamalia walio na mnasaba na twiga)
Jenasi: Okapia (Okapi)
Lankester, 1901
Spishi: Okapia johnstoni
Sclater, 1901

Usambazaji wa okapi

Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru

Okapi (Okapia johnstoni) ni mamalia wa familia ya twiga. Umbo lake hufanana na farasi ina michoro miguuni kama punda milia lakini haina uhusiano naye ni aina ya twiga.

Okapi ni mnyama aliyejulikana na wenyeji wa maeneo yao tu hadi mwaka 1901. Hapo zamani ilikuwa inaaminika kuwa mnyama huyu hupatikana tu katika misitu ya Ituri lakini mwaka 2006 zilipatikana dalili zilizoonyesha kwamba mnyama huyu yuko pia kwenye misitu ya hifadhi ya kitaifa ya Kongo ya Virunga. Kwenye misitu ya Ituri kuna hifadhi ya okapi yenye eneo la 14,000 km².

Shingo yake ni fupi kuliko twiga lakini ina ulimi mrefu sana wa kujipatia majani unaomwezesha kusafisha masikio yake yeye mwenyewe. Dume ina pembe mbili fupi kichwani.

Ukubwa wa okapi ni hadi mita 2.5 kichwani na hadi mita 2 mabegani. Anafikia uzito kati ya kg 200 hadi 250. Anakula majani ya miti pamoja na manyasi, matunda na nyoga.


Viungo vya nje

Picha

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

This article is issued from Wikipedia - version of the 10/26/2014. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.