Ono

Ono ni hali inayompata binadamu au mnyama kwa ndani, lakini inajitokeza kwa nje (inaonekana).

Ni tofauti na hali ya makusudi, kwa kuwa linasababishwa na jambo fulani.

Ndiyo maana katika Kiingereza linaitwa passion, neno la mkopo kutoka lile la Kilatini passio linalotokana na kitenzi patior (kupatwa).

Maono ni mbalimbali, lakini yale ya msingi ni: upande mmoja pendo (kwa jambo fulani), linalosababisha hamu (ya jambo hilo) na hatimaye furaha (jambo likipatikana); upande mwingine chuki (kwa jambo fulani), linalosababisha hofu (ya jambo hofu), hasira (dhidi ya hilo) na hatimaye huzuni (jambo likipatikana).

This article is issued from Wikipedia - version of the 3/9/2013. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.