Choroa

Choroa

Choroa beisa
(Beisa oryx)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Hippotraginae (Wanyama wanaofanana na korongo)
Brooke, 1876
Ngazi za chini

Jenasi 2:

Addax (Choroa adaksi) Laurillard, 1841
Oryx (Choroa) de Blainville, 1816

Spishi 5:

A. nasomaculatus (de Blainville, 1816)
O. beisa Rüppell, 1835
O. dammah Cretzschmar, 1827
O. gazella (Linnaeus, 1758)
O. leucoryx Pallas, 1766

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Choroa ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Addax na Oryx katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi O. beisa callotis, nususpishi O. b. beisa ilikuwa ikiitwa bara bara. Siku hizi spishi zote za Oryx huitwa choroa. Wanatokea maeneo makavu (jangwa na nyika) katika Afrika na Bara Arabu. Wana pembe ndefu nyembamba na nyofu au zilizopindika kidogo. Rangi yao ni ya mchanga au takriban nyeupe na wana mabaka meusi kichwani na miguuni, lakini choroa wa Sahara hana mabaka meusi. Wanyama hawa wanaweza kuendelea bila maji kwa wiki nyingi, kwa sababu huzidi halijoto ya mwili wao kuzuia kutoa jasho, na mkojo wao ni mzito sana. Hula manyasi, majani na matunda.

Spishi

Picha

Marejeo

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Choroa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

This article is issued from Wikipedia - version of the 11/11/2014. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.