Sauti

Sauti hutoka kwenye chanzo mfano ngoma.

Sauti (kutoka ar. صوت saut) inamaanisha kile tunachosikia kwa masikio yetu.

Kifizikia sauti ni uenezaji wa mabadiliko ya densiti na shinikizo katika midia kama kiowevu, gesi au gimba manga kwa njia ya wimbisauti.

Mchakato wa kusikia sauti

Kwa mfano kama mtu anapiga makofi mikono yake inasukuma hewa na kuikandamiza kati ya makofi. Wakati wa kukutana kwa makofi molekuli zinasukumwa kando. Mwendo huu wa ghafla unabadilisha densiti ya hewa karibu na mikono. Hewa ni midia nyumbufu yaani ikipigwa na nguvu fulani inabadilika hali yake lakini inataka kurudi katika hali yake ya awali. Tabia hii ya unyumbufu inaendeleza mabadiliko ya densiti na shinikizo ndani ya hewa kama mitetemo au wimbisauti. Kwa lugha nyingine tunasema "sauti inaenea".

Wakati mitetemo ya hewa iliyosababishwa na pigo la makofi inafikia katika sikio inaleta hapa mtetemeko kwa kiwambo cha sikio ambacho ni ngozi inayotikisishwa na mitetemo ya sauti. Neva ya sikio inabadilisha mwendo huu kwa mpwito wa umeme unaopelekwa kwenye sehemu husika ya ubongo. Kwa lugha nyingine "tunasikia sauti".

Nguvu ya mshtuko wa asili unaosababisha sauti inapungua katika mwendo wa uenezaji. Yaani nishati ya mshtuko wa kwanza inaendelea pande zote na kugusa molekuli nyingi zaidi kadri jinsi inavyoenea mbali na chanzo. Kwa hiyo nishati inayopatikana kwa kila molekuli inapungua. Hapa tunasema ya kwamba sauti ya karibu ni kali lakini sauti ya mbali ni dhaifu.

Midia na sauti

Ilhali sauti ni mwendo wa wimbisauti katika midia fulani hakuna sauti pasipo na midia. Katika anga la nje tukifika kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa ardhi hakuna sauti tena kwa sababu hakuna hewa au midia nyingine ya kupitisha mitetemo. Ila tu ndani cha chombo cha angani kuna midia tena kama hewa au ukuta metalia ya chombo chenyewe.

Sauti inaenea pia katika maji au ndani ya metali kama bomba au pau za feleji za reli. Uenezaji wa sauti katika midia mbalimbali ni tofauti kati ya midia na midia. Sauti inaenea haraka katika metali na maji kuliko hewa.

Sauti na marudio

Aina za sauti hutofautishwa kutokana na kiwango cha marudio yake:

Maelezo

  1. uwezekano huu unategemea utekelezaji safi wa ujenzi wa reli. Ni lazima ya kwamba pau za feleji zinagusana; kama kuna mapengo makubwa sauti haipiti
This article is issued from Wikipedia - version of the 11/12/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.