Sayansi

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli zilizo bainishwa pasi kuthibitishwa.

Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.

Aina za Sayansi

Mtu aliyerushwa hadi angani. Kufikia katikati ya Karne ya 20 binadamu ameweza kukua kisayansi na hivyo kuvumbua teknolojia zilizomwezesha kuruka na kuelea anga za juu kabisa za Dunia kwa mara ya kwanza na kuchunguza spezi.

Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika:

Sayansi Asili k.m.

Sayansi Umbile k.m.

Sayansi Jamii k.m.

Sayansi Tumizi k.m.

Pia, kuna sayansi zinahusu mada mbalimbali:

Charles Darwin mwaka 1854, alipokuwa anatunga kitabu chake On the Origin of Species.

Metodi za Kisayansi

Msingi wa sayansi ni vitendo.

Vitendo vya Kisayansi vina njia zake zinazotumikia kusimamisha kweli ya kisayansi.

Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka Nadharia ama Udhanifu. Halafu tena ili Kweli ikubalike; hutoka kwenye udhanifu; kwa kupitia kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.

Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaumba nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hii. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa ni nadharia inayokubalika.

Sura ya Kisayansi

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kuwa pingifu ya Hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika Jiwe (Maada Yabisi) kuna uvungu ( dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

Historia

Picha ya dunia ikionyesha kutokea kwa mabara kutoka kugawanyika kwa Pangea mpaka hivi leo.

Sura ya Kiutamaduni

Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmoja mmoja; lakini kadri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wakujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo ilionekana kama ni shauku la mtu mmoja mmoja kama awali. Aristotle, 384 BC – 322 BC - alichangia katika ukuaji wa sayansi.]]


Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa ni sehemu ya historia ya Sayansi. Majina na sifa kutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.

Sayansi na Jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

Sayansi na Siasa za dunia

Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.

Ingawaje haibanishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu kimamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.

Sayansi na Maendeleo

Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu kuwa mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.

mambo mbalimbali ya kikemikali yaliyosomwa na Michael Faraday na kuripotiwa katika historia yake kabla ya mamlaka ya kisheria: Historia ya kikemilkali ya mshumaa, mwaka 1861

Na hivyo roho ya uchunguzi ndio iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sayansi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article is issued from Wikipedia - version of the 8/6/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.