Washia

Nchi za Waislamu wengi na madhehebu
Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Historia ya Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Nguzo za Kiislamu
Shahada Swala Saumu
Hija Zaka

Watu muhimu

Muhammad

Abu Bakr Ali
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'an Sunnah Hadithi
Sheria Kalam
Wasifu wa Muhammad
Sharia

Aina za Uislamu

Sunni Shi'a Kharijite

Tamaduni za Kiislamu

Shule Historia
Tauhidi Falsafa Sayansi
Sanaa Ujenzi Miji
Kalenda Sikukuu
Wanawake
Viongozi Siasa
Umma Itikadi mpya Sufii

Tazama pia

Kamusi Kuogopa Uislamu

Washia (pia: Shi'a; kutoka Kiarabu:شيعة) ni dhehebu katika Uislamu. Kufuatana makadirio mbalimbali kati ya asilimia 10 na 20 za Waislamu wote hufuata Shia na wengine walio wengi ni Wasunni.

Lakini katika nchi za Uajemi, Azerbaijan, Iraki, Bahrain, Yemen, Omani na Lebanoni Washia ndio kundi kubwa.

Neno Shia latokana na Kiarabu shiá't ali (شیعته علی) yaani "chama cha Ali" likimaanisha kundi la wafuasi wa Ali ibn Abu Talib aliyekuwa mkwe wake Mtume Muhammad na familia yake.

Chanzo cha Shia

Washia huamini ya kwamba familia ya Muhammad hustahili kuwa na uongozi kati ya Waislamu. Familia hii huitwa "ahl-al-bayt" (Kiarabu:أهل البيت).

Ali alimwoa mtoto wa pekee wa mtume aliyeishi yaani binti yake Fatima akawa pia baba wa Hassan na Husain wajukuu wa pekee wa mtume . Baada ya kifo cha Ali wafuasi wake walitaka Hasan na Husein kumfuata katika nafasi ya uongozi wa Uislamu wote lakini idadi kubwa ya Waislamu walishikamana na Muawiya

Washia huamini ya kwamba uongozi wa ahl-al-bayt uliendelea kupitia maimamu mbalimbali.

Vikundi

Washia waligawanyika baada ya imamu wa sita Ismail ibn Dschafar kuhusu swali ni nani imamu halali wa saba. Kutokana na farakano hili vikundi mbalimbali vilijitokeza.

Kutokana na uhamiaji wakati wa karne ya 19 matawi ya Waismaili yamepatikana pia katika Afrika ya Mashariki. Hasa Wakhodja wamejitolea katika mazingira wanapoishi kwa kujenga shule, sahanati na mahospitali vinavyoitwa mara nyingi "Aga Khan".

Kihistoria palikuwa na vikundi vingi vingine kama vile Wafatima waliotawala Misri kati ya 953 na 1171 BK.

Viungo vya Nje

This article is issued from Wikipedia - version of the 3/11/2013. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.