Nyati wa Afrika

Nyati wa Afrika

Nyati katika Hifadhi ya Mabula, Afrika Kusini
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Bovinae (Wanyama wanaofanana na ng'ombe)
Jenasi: Syncerus (Nyati)
(Hodgson, 1847)
Spishi: S. caffer
(Sparrman, 1779)
Ngazi za chini

Nususpishi 5:

S. c. aequinoctialis Blyth, 1866
S. c. brachyceros J. E. Gray, 1837
S. c. caffer Sparrman, 1779
S. c. mathewsi Lydekker, 1904
S. c. nanus Boddaert, 1785

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyati au mbogo (Syncerus caffer) ni mnyama mkubwa wa Afrika. Hana uhusiano wa karibu na nyati-maji wa Asia aliye kubwa zaidi kidogo, lakini asili yake haieleweki. Kutokana na tabia yake isiyotabirika na inayomsabibisha kuwa hatari sana kwa binadamu, nyati hafugwi kinyume na mwenzake wa Asia.

Maelezo

Nyati ni mnyama mkubwa. Ana mita 1.7 juu, urefu wa mita 3.4. Nyati wa savana ana uzito wa kilo 500–900, ambapo nyati wa kiume kwa kawaida huwa mkubwa kuliko nyati wa kike, akiwa na uzito wa juu mbalimbali. Nyati wa msitu huwa nusu wa kiwango hicho.[1] Nyati wa savana huwa wa rangi nyeusi au kahawia nyeusi na pembe zao zimejikunja katika mpevu; nyati wa msitu nao huwa wa rangi ya kahawia nyekundu na pembe zao zimejikunja nyuma na juu. Ndama wa aina zote mbili wana ngozi nyekundu.

Nususpishi

Mazingira

Kundi la nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania.

Nyati wa Afrika ni mmjoa wa wanyama maarufu walao nyasi katika Afrika. Waishi katika maeneo ya vinamasi, mbuga, na misitu za milima mikuu ya Afrika. Nyati hupendelea makazi ya vichaka au matete manene, lakini wapatikana pia katika mapori wazi. Makundi makubwa ya nyati hupatikana katika maeneo ya miti na mapori. Nyati huhitaji maji kila siku, kwa hiyo wategemea vyanzo vya kudumu vya maji.

Kama punda milia, nyati hula manyasi marefu. Nyati hupunguza urefu wa nyasi ili zapendelewa na wanyama wengine walao nyasi. Wakati kula, nyati hutumia ulimi na meno yake mapana kula nyasi haraka kuliko wanyama wengine wa Afrika walao nyasi. Nyati hawakai katika maeneo yaliyokanyagwa au kupunguzwa kwa muda mrefu.

Zaidi na binadamu, nyati huwa na adui chache na wana uwezo wa kujikinga na simba, na hata kumwua.[2] Simba huwaua na kula nyati mara kwa mara, lakini kwa kawaida huchukua simba wengi kumwangusha nyati mzima mmoja. Mamba wa Nile kwa kawaida hushambulia nyati wazee na ndama tu.[3] Chui na fisi ni tisho tu kwa ndama mchanga, ingawa fisi wamerekodiwa kumwua nyati mzima wakati mwingine.[4]

Tabia za kijamii

Ukubwa wa makundi ya nyati hubadilika sana. Makundi ya kawaida huwa na nyati wa kike wanaohusiana, pamoja na uzao wao, katika ukoo ambao hupangwa kwa hadhi. Makundi ya kawaida huzungukwa na makundi madogo ya madume ya cheo cha juu, madume ya chini, majike ya cheo cha juu na walio wazee. Madume vijana hukaa mbali na fahali atawalaye, ambaye hujulikana kutokana na ukubwa wa pembe zake.

Mafahali wanaoandaa kushindana.

Mafahali wazima hushiriki katika michezo ya kupigana au vita halisi. Fahali mmoja atakaribia mwenzake, akikoroma, kichwa chake chini, na kusubiri mwenzake kufanya hivyo. Mafahali hao wanapopigana hugeuza pembe zao kushoto na kulia. Ikiwa vita hivyo vina madhumuni ya kucheza, mafahali husuguana uso na miili katika mchezo huu. Vita halisi ni kali, lakini ni nadra na vifupi. Ndama pia wanaweza kushindana, lakini ni nadra kwa nyati wa kike kushindana hivyo.

Wanapokimbizwa na wanyama wa kuwinda, nyati hukaa pamoja kufanya kuwa ngumu kwa wanyama wa kuwinda kunyang'anya mmoja wao. Ndama hukusanyika katikati. Nyati atajaribu kumnusuru mwenzake aliyeshikwa. Wito wa ndama hupata uangalifu wa mama na pia kundi lote. Nyati hupigana wakiwa wengi wanapopigana na wanyama wa kuwinda. Wamerekodiwa kuwakimbiza simba juu ya mti na kuwasumbua kwa masaa mawili, baada ya simba kuua nyati mwenzao. Inawezekana kwa watoto wa simba kukanyagwa na kuuawa na nyati. Katika tukio lililochukuliwa na picha, ndama alinusurika aliposhambuliwa na simba wachache na mamba baada ya kusaidiwa na kundi.

Uzazi

Nyati wa Afrika na ndama wake.

Nyati hujamiiana na kujifungua wakati wa mvua pekee yake. Kilele cha kuzaa huwa mwanzoni wa msimu na kilele cha kujamiiana huwa baadaye. Fahali atakaa karibu na nyati aliye na joto na pia kuweka mafahali wenzake mbali. Hii ni vigumu kabisa kwani nyati huwavutia wanaume wengi katika eneo hilo. Wakati ng'ombe ako tayari kamili, fahali tu aliye na nguvu kabisa ndiye hubakia kule.

Majike huzaa mara ya kwanza baada ya miaka mitano, baada ya kipindi cha mimba miezi 11.5. Ndama waliozaliwa hufichwa katika vichaka kwa wiki chahe za kwanza wakitunzwa na mama zao kabla ya kujiunga na kundi kuu. Ndama huwa katikati ya kundi kwa ajili ya usalama.[5] Uhusiano wa mama na ndama hudumu muda mrefu zaidi kuliko wanyama wengi walao majani. Hata hivyo wakati ndama mpya anapozaliwa, ule uhusiano unaisha na mama yake huwaweka mbali watoto wengine kutumia pembe. Nyati wa kiume huacha mama zao wanapokuwa na umri wa miaka miwili na kujiunga na vikundi vya mafahali walio wachanga.

Uhusiano na binadamu

Nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Tanzania.

Hali

Hali ya sasa ya nyati wa Afrika hutegemea kuwepo kwa thamani wawindaji wa wanyama na watalii wawindaji, wakiingilia harakati za kuhifadhi kupitia doria ya urekebishaji wa uharibifu wa mazao kijijini, na programu za marekebisho ya maeneo ya CAMPFIRE.

Nyati wafugwao nchini Kenya katika jua kuchwa.

Idadi jumla ya nyati imeenea eneo zote zisizo jangwa katika Afrika, kutoka kusini ya Chad mpaka Afrika ya Kusini. Idadi ya nyati inakadiriwa karibu milioni moja, lakini hesabu sahihi haiwezekani kwani hakuna usaidizi wa fedha za utafiti katika maeneo kama vile Sudan, Chad, Congo, na Benin. Wengi wa wawindaji wataalamu, wanaosafiri, na wataalamu wa wanyamapori huamini kuwa idadi hii inawakilisha nyati kusi, bila kuhesabu nyati wa naili, nyati-milima, au nyati-msitu.

Mashambulizi

Kama mmoja wa "Wakubwa tano" au "Kifo cheusi" katika Afrika, nyati wa afrika anajulikana kama mnyama hatari sana, wakiua watu zaidi ya 200 kila mwaka. Nyati wakati mwingine huripotiwa kuua watu zaidi katika Afrika kuliko mnyama mwingine wowote, ingawa wakati mwingine hudaiwa kusababishwa na kiboko, au mamba.[6] Nyati huwa na sifa mbaya miongoni mwa wawindaji kama mnyama hatari sana, kwa sababu ya wanyama waliojeruhiwa wakiripotiwa kuvizia na kushambulia wawindaji.[7]

Picha

Angalia pia

Marejeo

  1. Syncerus caffer.
  2. Cape Buffalo. Canadian Museum of Nature.
  3. [5] ^ Syncerus caffer - Nyati wa Afrika
  4. Kruuk, Hans (1972). The Spotted Hyena: A study of predation and social behaviour. New York: Parkwest, 335. ISBN 0563208449.
  5. African Buffalo. British Broadcasting Corporation. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-07-28.
  6. Africa on the Matrix: The Cape Buffalo.
  7. African Animals Hunting facts and tips - Buffalo Hunting.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nyati wa Afrika


Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/22/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.