Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa (UM) ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru.

Umoja huu ulianzishwa mwaka 1945 na nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia; zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2013 kulikuwa na nchi 193 wanachama, mbali na Ukulu mtakatifu (Vatikani) na Palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura.

Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k.

Toka mwanzo makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York nchini Marekani.

Umoja huu ulichukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa (1919 - 1946).

Lugha rasmi za UM ni sita: Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi na Kihispania.

Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni Ban Ki-moon kutoka Korea ya Kusini. Ban Ki-moon alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka 2006 akichukua nafasi ya Kofi Annan, akaongezewa kipindi kingine tena.

Muundo wa UM

Ukumbi wa UM.

UM una vyombo vitano:

Cha sita kilikuwa Baraza la Wafadhili la UM (Trusteeship Council), ambacho kimesimamisha kazi yake 1994.

Baraza la Usalama linaamua kutuma walinzi wa amani wa UM penye maeneo ya ugomvi.

Vyama vya pekee vya UM

Viungo vya Nje

Official website

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/22/2015. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.