Wakati

Saa ya mfukoni


Wakati ni neno la kutaja ama ufuatano wa matokeo au muda ama kipindi ambamo jambo latokea.

Tunaishi katika wakati na tunapanga maisha yetu kufuatana na wakati lakini si rahisi kusema wakati ni kitu gani. Sayansi, fizikia, falsafa na dini zote zina njia mbalimbali za kuangalia na kueleza wakati.

Wakati kama mpito

Katika maarifa ya kila siku wakati ni utaratibu wa mfululizo wa matokeo. Tunaweza kuona ya kwamba jambo liliwahi kutokea (wakati uliopita), linaendelea sasa (wakati wa kisasa) na tunatarajia litaendelea katika wakati ujao. Hivyo ndivyo tunatazama maisha yetu tukikumbuka mambo yaliyopita, tunasikia hali au mambo yanayoendelea na kutegemea kuona siku inayokuja.

Kwa sababu hiyo kuna usemi kama "wakati unapita" au "wakati unakimbia".

Wakati kisayansi

Sayansi hutumia wakati kwa vipimo vingi hata kama haijui wakati mwenyewe ni kitu gani. Imeunda vipimo vya wakati mwenyewe vinavyowezesha kuelewa matokeo na kuyalinganisha.

Hapa sayansi inajaribu kuona wakati kama wanda (dimensioni) moja ya ulimwengu pamoja na zile tatu za nafasi ya ulimwengu. Hapa huitwa "wanda ya nne" (the fourth dimension).

Tofauti yake na nyanda za nafasi ni ya kwamba wakati una mwendo na mwelekeo.

Vipimo vya kawaida vya wakati

Vipimo vya wakati hutumia matokeo yanayorudia mara kwa mara bila mabadiliko.

Kipimo cha kawaida ni siku au kwa lugha nyingine muda wa mzunguko 1 wa dunia yetu unaonekana kwetu kutokana mabadiliko ya mchana na usiku.

Muda huu wa Mzunguko mmoja hugawiwa kwa masaa 24 na kuitwa "siku". Saa hugawiwa kwa dakika 60 na kila dakika kwa sekunde 60.

Mbio mmoja wa dunia yetu kuzunguka jua huitwa "mwaka". Utaratibu wa miaka hupangwa kwa njia ya kalenda.

Vipindi kama mwezi na wiki hupanga siku ndani ya kalenda.

Saa atomia

Vipimo vya Kisayansi

Sayansi haijaridhika tena na vipimo hivi vya kawaida. Mizunguko ya dunia au siku hazilingani kikamilifu. Hapa sayansi imeondoka katika siku kama msingi wa vipimo bya wakati. Badala yake imechukua muda wa sekunde na kukiliganisha kwa mwendo wa atomi.

Katika vipimo sanifu vya kimataifa sekunde imewekwa kama muda wa radidi (periodi) 9,192,631,770 za mnururisho wa atomi ya caesi ya 133Cs.

Vipindi vya wakati

Viungo vya Nje

This article is issued from Wikipedia - version of the 4/17/2016. The text is available under the Creative Commons Attribution/Share Alike but additional terms may apply for the media files.